Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisons yagoma kushuka, yaichongea Fountain Gate

Muktasari:

  • Msimu wa 2021-2022 Prisons ilinusurika pia kushuka daraja kupitia play-off dhidi ya JKT Tanzania kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, baada ya kushinda ugenini 1-0 na kupata sare ya 1-1 nyumbani. Awali katika msimu huo ilinyooshwa na Mtibwa Sugar kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda ugenini 1-0 na kufungwa nyumbani mabao 3-1.

MAAFANDE wa Tanzania Prisons wamegoma kushuka daraja kwa mara nyingine baada ya kuifumua Fountain Gate mabao 3-1 katika mechi ya marudiano ya play-off iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Msimu wa 2021-2022 Prisons ilinusurika pia kushuka daraja kupitia play-off dhidi ya JKT Tanzania kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, baada ya kushinda ugenini 1-0 na kupata sare ya 1-1 nyumbani. Awali katika msimu huo ilinyooshwa na Mtibwa Sugar kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda ugenini 1-0 na kufungwa nyumbani mabao 3-1.

Matokeo ya mechi ya jana yameifanya Prisons kusalia katika Ligi Kuu kwa msimu ujao kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara na kuwaachia msala Fountain kwenda kucheza na Stand United.

Stand iliyomaliza nafasi ya nne katika Ligi ya Championship, itavaana na Fountain Julai 3 mjini Shinyanga ili kusaka nafasi ya kupanda Ligi Kuu kwa msimu ujao kuzifuata Mtibwa Sugar na Mbeya City na kuwashusha wapinzani wao hao watakaoungana na KenGold na Kagera Sugar.

Lakini kama itachemsha itaifanya Fountain kusalia katika Ligi Kuu na Chama la Wana kusalia Ligi ya Championship kwa mara nyingine.

Katika mechi ya leo iliyochezeshwa na mwamuzi Amina Kyando, Prisons ilipata mabao yake kupitia na Beno Ngassa aliyefunga dakika ya nane tu ya mchezo kwa kichwa kuwahi mpira wa krosi ya Oscar Mwajanga kabla ya Ezekia Mwashilindi kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya kipa wa Fountain kumpiga kiwiko Haruna Chanongo na kulimwa kadi nyekundu kabla ya kutolewa adhabu hiyo sekunde chache kabla ya mapumziko. Hata hivyo, bao hilo lilikuja baada ya Fountain kuchomoa bao la kwanza la Prisons lililowekwa kimiani na beki Laurian Makame dakika ya 28.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na wenyeji Prisons kupata bao la tatu dakika ya 48 kupitia kwa Mwashilindi tena, huku Fountain ikipoteza penalti katika kipindi hicho na kuikatisha tamaa timu hiyo.

Fountain sasa inajiandaa kuanza safari kwenda Shinyanga kukabiliana na Stand iliyoifumua Geita Gold katika play-off ya Ligi ya Championship, mechi hiyo ya kwanza inapigwa Julai 3 kabla ya kurudiana mjini Babati Julai 7 na kujulikana mbabe.