Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pluijm aikomalia Yanga

Muktasari:

  • Yanga iliachana na Pluijm msimu wa 2017/18 kumchukua Mzambia, George Lwandamina kisha akaenda nzake Singida United na baadaye msimu huu Azam kwa mkataba wa mwaka mmoja uliositishwa na mabosi wa klabu hiyo.

HAKUNA ubishi Yanga ndio iliyompa ujiko Kocha Hans Pluijm na kumtambulisha kwa mashabiki wa soka nchini ilipoingia naye karandarasi ya kuinoa Januari 2014, kitu hicho kumbe bado kipo akilini mwa Mholanzi huyo na kudai haiwezi kuitosa jumla klabu hiyo.

Pluijm alisema licha ya kujivunia mafanikio aliyoyapata Yanga, lakini anaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa klabu hiyo na ataendelea kuwasiliana nayo kokote alipo baada ya kutemana na Azam FC.

Yanga iliachana na Pluijm msimu wa 2017/18 kumchukua Mzambia, George Lwandamina kisha akaenda nzake Singida United na baadaye msimu huu Azam kwa mkataba wa mwaka mmoja uliositishwa na mabosi wa klabu hiyo.

“Kuondoka Tanzania haimaanishi ndio mwisho wa uhusiano wangu na Yanga, nimetokea kuipenda kutoka moyoni sio tu kwa sababu niliifundisha bali imenipa heshima kubwa nilichukua kadi kwa kumanisha na sio mihemko.

Kubwa zaidi nitaendelea kuwa na mawasiliano ya karibu sana na yule ambaye ndiye alifanikisha kutua Yanga mara ya kwanza lakini mashabiki ambao waliniunga mkono katika kazi zangu, ipo kichwani na moyoni haitafutika.”