Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pique avunja ukimya sakata la Shakira

Muktasari:

Wiki iliyopita kulikuwa na uvumi kuhusu mastaa hao kutengana jambo ambalo lilizua gumzo mtandaoni.

Gerrard Pique amewajibu wabaya wake wanampakazia kuhusu kutengana na mkewe Shakira baada ya kuibukia katika mazoezi ya mwanamuziki huyo nyota duniani.

Kwa takribani wiki kadhaa kumekuwa na taarifa za beki huyo wa kimataifa wa Barcelona na Hispania kutengana na mkewe waliyezaa watoto wawili.

Lakini kwa mara ya kwanza, mchezaji huyo amevunja ukimya kwa kuweka picha ikimuonyesha akiwa kwenye mazoezi ya Shakira.

Mashabiki wa soka Hispania wamekuwa wakimdhihaki Pique uwanjani kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na Shakira, lakini hakuwahi kuwajibu.

Picha hiyo inamuonyesha Pique akiwa ameweka kidole mdomoni ikiwa ni ishara ya kuwataka wabaya wake kukaa kimya huku Shakira akiendelea na mazoezi.

Pique na Shakira walianzisha uhusiano mwaka 2010 nchini Afrika Kusini wakati mwanamuziki huyo alipokwenda kutengeneza wimbo wa Kombe la Dunia.

 

Mchezaji huyo alianza kuonja shubiri, baada ya kupaza sauti akitaka kujitenga kwa Jimbo la Catalunya, kauli ambayo imeibua hisia kubwa kwa mashabiki wa soka nchini humo.