Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Exim Bank yaipa nguvu Kitonga Marathon

MARATHON Pict

Muktasari:

  • Mbio hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu ya “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo” zilikutanisha washiriki na wadau mbalimbali katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na kuibua fursa za uwekezaji katika sekta za kilimo, utalii na biashara.

BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kuunga mkono maendeleo ya jamii kupitia udhamini wake mkuu wa Kitonga Marathon 2026, mashindano yaliyolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Mbio hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu ya “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo” zilikutanisha washiriki na wadau mbalimbali katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na kuibua fursa za uwekezaji katika sekta za kilimo, utalii na biashara.

Kupitia udhamini huo, Exim Bank imeonyesha dhamira yake ya kutumia michezo kama jukwaa la kuunganisha jamii, kuhamasisha maendeleo na kutoa nafasi ya kutangaza uwezo wa kiuchumi wa maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumzia ushiriki wa benki hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Exim Bank Tanzania, Stanley Kafu, amesema udhamini huo ni sehemu ya wajibu wa taasisi hiyo katika kuchangia maendeleo ya jamii zaidi ya huduma za kifedha.

Amesema mbio hizo ni fursa muhimu ya kuitangaza Kilolo na kuhamasisha ushirikiano katika kulinda mazingira na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo ya wananchi.

“Mbio za Kitonga zinatoa fursa ya kuitangaza zaidi Kilolo na uwezo wake wa kiuchumi, huku zikihamasisha uwajibikaji wa pamoja katika uhifadhi wa mazingira.

“Sisi Exim Bank tunaamini maendeleo endelevu yanahitaji ushirikiano kati ya jamii, wafanyabiashara na wadau wengine. Udhamini wetu unaakisi dhamira ya kushirikiana na jamii tunazozihudumia na kuchangia juhudi zinazolenga kuleta maendeleo katika maeneo yao,” amesema Kafu.

Udhamini wa Kitonga Marathon ni sehemu ya mpango wa uwajibikaji kwa jamii wa benki hiyo unaojulikana kama Exim Cares, unaolenga kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali ikiwamo afya, elimu, uhifadhi wa mazingira, ubunifu na elimu ya masuala ya fedha.

Katika kuendeleza dhamira hiyo, mwaka huu Benki ya Exim ilifanya shughuli za usafi katika maeneo yanayozunguka matawi yake nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kuanzishwa kwake.

Mkoani Iringa, wafanyakazi wa tawi la benki hiyo walikabidhi vifaa vya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Flerimo kwa lengo la kusaidia kuboresha mazingira ya huduma za afya.

Exim Bank ilifungua tawi lake mkoani Iringa mwaka 2009 na tangu wakati huo imeendelea kutoa huduma za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara, kampuni na taasisi mbalimbali.

Ushiriki wake katika Kitonga Marathon unaendeleza ushirikiano huo na jamii ya Iringa, huku ukionyesha namna taasisi za kifedha zinavyoweza kutumia majukwaa ya michezo kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kwa upande mwingine, benki hiyo imeendelea kutoa huduma mbalimbali kupitia matawi yake na mifumo ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na kuwapatia wateja ushauri kuhusu mahitaji yao ya kifedha.