Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba Jiji yamtema Arjif Ali Amour

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti Arjif aliyejiunga na Pamba kama mchezaji huru Agosti 7, 2025 akitokea Azam FC, yupo hatua za mwisho za kusitishiwa mkataba wake uliobakia.

MABOSI wa Pamba Jiji wako katika mazungumzo ya kusitisha mkataba na kipa wa timu hiyo, Arjif Ali Amour, baada ya nyota huyo aliyekitumikia kikosi hicho kwa mkataba wa miezi sita, kushindwa kupigania nafasi na makipa wengine walio kikosini.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti Arjif aliyejiunga na Pamba kama mchezaji huru Agosti 7, 2025 akitokea Azam FC, yupo hatua za mwisho za kusitishiwa mkataba wake uliobakia.

“Lengo letu ni kuondoa wachezaji ambao tunaona wameshindwa kushindania nafasi na wengine, ni kipa mzuri ila kutokana na umri wake tunataka kumuacha ili akapate timu itayomsaidia kuonekana na kuboresha kiwango chake,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Pamba, Ezekiel Ntibikeha, amesema baada ya kupitia ripoti ya benchi la ufundi ndipo watafanya uamuzi wa mwisho wa wachezaji watakaobaki au kuondoka hivyo, kwa sasa bado ni mapema juu ya hilo.

“Dirisha la usajili bado halijafunguliwa lakini tunajua tunatakiwa kufanya nini kutokana na ripoti ya kocha atakayotupa, wapo wachezaji tutakaoachana nao ili wakatafute changamoto mpya, ingawa tutaweka wazi muda ukifika,” amesema Ntibikeha.

Nyota huyo aliyejiunga na Azam Agosti 15, 2024, akitokea KVZ ya visiwani Zanzibar, ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo na hata alipojiunga pia na Pamba, hivyo kufunguliwa mlango wa kutokea dirisha hili dogo.

Arjif ni nyota wa nne kutemwa baada ya Abdallah Kheri ‘Sebo’ aliyetua Singida Black Stars, Saleh Masoud Abdallah ‘Tumbo’ anayedaiwa kujiunga Fountain Gate na mshambuliaji, Abdallah Idd ‘Pina’ aliyejiunga na Muembe Makumbi City ya Zanzibar.