Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba Jiji yaanza mkwara

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Pamba Jiji ilikuwa na msimu bora uliopita ikionesha soka la ushindani na kufanikiwa kumaliza nafasi ya saba kwa pointi 36 na tayari imeanza kambi kujiwinda na msimu ujao chini ya Kocha wake, Francis Baraza raia wa Kenya.

ACHANA na kuondokewa baadhi ya nyota wake waliokuwa wakianza kikosi cha kwanza, Pamba Jiji imesema inasuka upya timu hiyo na msimu ujao makali yao yatakuwa ni zaidi ya msimu uliopita.

Pamba Jiji ilikuwa na msimu bora uliopita ikionesha soka la ushindani na kufanikiwa kumaliza nafasi ya saba kwa pointi 36 na tayari imeanza kambi kujiwinda na msimu ujao chini ya Kocha wake, Francis Baraza raia wa Kenya.

Hata hivyo hadi sasa takribani wachezaji sita wameondoka kikosini humo baada ya kutakiwa na timu nyingine wakiwa ni kipa Yona Amos na kiungo, James Mwashinga na straika Methew Tegis waliojiunga na Singida Black Stars.

Hata hivyo, timu hiyo tayari imeshanasa nyota wapya saba ikiwa ni Aly Machupa kutoka Namungo, Frank Ernest, Kipa Erick Johora na Nonyem Okorocha raia wa Nigeria aliyetokea Mlandege FC na Saleh Karabaka kutoka JKT Tanzania na kipa Steve Ochieng kutoka Shabana ya Kenya.

Afisa Habari wa timu hiyo, Moses Wiliam amesema kuondoka kwa nyota wao ni sababu mbalimbali ikiwamo uamuzi wa wao wenyewe, kumaliza mikataba na mapendekezo ya benchi la ufundi.

Amesema kwa sasa timu hiyo inaendelea na usajili kulingana na mahitaji na mapendekezo ya kocha Baraza, akieleza kuwa wanaamini watatengeneza kikosi kipya chenye ubora hata zaidi ya msimu uliopita.

“Hatujapoteza mwelekeo, kocha anaendelea kusuka kikosi kama ilivyokuwa msimu ulioipita, usajili tunaoufanya ni mahitaji ya kocha na timu kwa ujumla, tunaamini tutakuwa imara zaidi” amesema Wiliam.

Ameongeza kuwa kwa sasa timu imeanza kambi kujiwinda na ligi kuu msimu ujao inayotarajia kuanza Agosti 14, akibainisha kuwa matarajio ni kusajili nyota wapya zaidi ya 10 kutokana na malengo yao.

“Tumona ratiba ya ligi kwetu tumefurahia kwa mechi tunazoanza nazo ndio maana timu ipo kambini kujiandaa, kimsingi wadau na mashabiki wetu wasubiri kuona maajabu yetu”ametamba Afisa huyo.