Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okwi atulizwa kiana

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ameshindwa kucheza katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prison jana kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa dakika ya pili na mshambuliaji Meddie Kagere aliyepokea pasi safi ya kisigono kutoka kwa nahodha John Bocco.

Okwi mfungaji bora wa msimu uliopita alikosekana mechi hiyo kutokana na kuwa na maumivu ya mgongo ambayo aliumia katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kocha wa Simba, Mbeligiji Patrick Aussems alisema ameshindwa kumpa nyota huyo nafasi ya kucheza kwa kuwa ana maumivu ya mgongo na bado hajapona vizuri na kama angelazimisha kumtumia angeweza kumkosa muda mrefu.

Aussems alisema Okwi aliumia mgongo katika mechi ya Mtibwa ambayo alishindwa kuendelea na alitoka nje maumivu ambayo anatakiwa kupata matibabu huku akipata muda mwingi wa kupumzika ili kupana haraka.

Anasema Okwi anaendelea vizuri na matibabu na alikuwa na uwezo wa kumtumia katika mechi hiyo, lakini kwa kuwa walikuwa mbele kwa bao moja aliona vyema kumpumzisha ingawa alikuwa katika benchi la wachezaji wa akiba.

"Tunamechi nyingi mbele yetu zinakuja ningeweza kumtumia akaja kutonesha maumivu au kuumia zaidi na tukamkosa kwa muda mrefu jambo ambalo lisengekuwa sahihi kwetu," alisema kocha huyo.

"Kikosi ni kipana kukosekana kwa Okwi nafasi yake amecheza mchezaji mwingine," alisema Aussems.