Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Ngorongoro Heroes hachezei fursa

SAGWE Pict

Muktasari:

  • Sagwe ni mmoja wa wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Ngorongoro Heroes akiisaidia timu hiyo kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana AFCON U-20 yatakayopigwa mwakani Ghana.

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya vijana U-20, Ngorongoro Heroes, Juma Sagwe amesema amekuwa akizitumia timu za vijana kuonyesha uwezo wake, akiamini kila fursa anayopata inaweza kuwa hatua muhimu katika safari yake ya soka.

Sagwe ni mmoja wa wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Ngorongoro Heroes akiisaidia timu hiyo kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana AFCON U-20 yatakayopigwa mwakani Ghana.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sagwe anayekipiga KMC, amesema kila anapopewa nafasi anataka kuitumia kwa kiwango kikubwa ili kutengeneza kujenga jina lake.

“Sina nafasi ya kuonekana zaidi ya kutumia fursa hizi za timu za vijana. Kila nafasi ninayoipata lazima nitumie vizuri ili inisaidie kwenye kazi yangu,” amesema Sagwe.

Mshambuliaji huyo alitolea mfano kwenye kikosi cha vijana U-17 na alitumia mashindano hayo kuonyesha uwezo wake na baadaye akapata nafasi ya kwenda Uturuki kufanya majaribio katika klabu ya Goztepe inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki.

“Mashindano ya U-17 yaliyopita nilijaribu kutumia vizuri nafasi nilizopata na nikapata fursa ya kwenda kufanya majaribio Goztepe. Ingawa sikupata nafasi ya kubaki, kwangu ilikuwa ni uzoefu mkubwa na imeniongezea kitu katika safari yangu,” amesema.

“Kila ninapopata nafasi nataka kuitumia vizuri. Mabao mawili ni mwanzo mzuri kwangu, lakini kikubwa kwangu ni kusaidia timu na kuonyesha kile ninachoweza.”