Nsajigwa awafuata jukwaani Yondani, Chirwa
Muktasari:
Nsajigwa alikuwa akitumikia adhabu hiyo baada ya kutolewa katika benchi katika mchezo ya marudiano dhidi ya Township Rollers.
Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alikuwa kukwaani kuangalia mechi ya timu yake dhidi ya Welayta Dicha pamoja na wachezaji wake Kelvin Yondani, Obrey Chirwa wakitumikia adhabu ya CAF.
Nsajigwa alikuwa akitumikia adhabu hiyo baada ya kutolewa katika benchi katika mchezo ya marudiano dhidi ya Township Rollers.
Hata hivyo Yanga walishtuka janja ya CAF, kwa sababu jukwaani hapa alikuwa amekaa na kocha wa viungo Noel Mwandila.
Yanga wanahofia kupata adhabu kwa kuwaweka makocha hao katika benchi, kwa sababu wanahisi kwamba aliyepewa adhabu ya kutokukaa katika benchi ni Noel Mwandila na siyo Shadrack Nsajigwa, hivyo wakaona wote wasikae katika benchi.
Wachezaji wengine Yanga waliokuwa jukwaani ni viungo Said Juma ‘Makapu’ na Papy Tshishimbi sambamba ambao wanatumikia adhabu ya kukosa mechi moja baada ya kupata kadi mbili za njano kwenye mechi mbili zilizopita za Ligi ya Mabingwa Afrika.