Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neema aipaisha Tanzania Kwibuka T20 Rwanda

NOELA Pict

Muktasari:

  • Neema nyota mpya ya kriketi kwa timu ya wanawake ya Tanzania alitangazwa ndiye mtengezaji bora wa mikimbio baada ya kupiga jumla 218 katika mechi nane ilizocheza Tanzania na kumfanya amalize akiwa na wastani wa mikimbio 36.33 kwa kila mechi.

Neema Pius alishirikiana vyema na Fatuma Kibasu kuifanya Tanzania kuibuka kinara wa  mikimbio katika michuano ya Kumbukumbu ya Kwibuka iliyomalizika wikiendi iliyopita, jijini Kigali, Rwanda.

Neema nyota mpya ya kriketi kwa timu ya wanawake ya Tanzania alitangazwa ndiye mtengezaji bora wa mikimbio baada ya kupiga jumla 218 katika mechi nane ilizocheza Tanzania na kumfanya amalize akiwa na wastani wa mikimbio 36.33 kwa kila mechi.

Neema ni mpigaji (batter) anayetumia mkono wa kulia.

Nafasi ya pili ilichukuliwa tena na Mtanzania, mchezaji mkongwe, Fatuma Kibasu aliyepiga jumla ya mikimbio 193 katika mechi nane na kuwa na wastani wa mikimbio  27.57 kwa kila mechi.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na  Marie Bimenyimana wa Rwanda aliyepiga 146 katika mechi nane na kuwa wastani wa mikimbio 20.85 kwa kila mechi.

Licha ya kufanya vizuri kwa upande wa upigaji mikimbio, Tanzania haikufanya vizuri kwenye wiketi na udhaifu huu ndiyo ulioifanya kupoteza dhidi ya Nigeria, Uganda na Zimbabwe.

Hata hivyo, Tanzania ndiyo timu ya pekee iliyowafunga wenyeji Rwanda kwa mikimbio 16 licha ya nchi hiyo kuibuka mshindi wa jumla wa michuano ya mwaka huu.

Tanzania ilimaliza nafasi ya nne nyuma ya Zimbabwe, Uganda na mabingwa Rwanda.  

Rwanda imemaliza na pointi 14  baada ya kushinda michezo saba na kupoteza mmoja dhidi ya Tanzania, huku Uganda ikimaliza ya pili na pointi 12 baada ya kushinda michezo sita na kufungwa miwili.

Zimbabwe ilishika nafasi ya tatu na pointi 12 sawa na Uganda, lakini ilishindwa kutokana ba uwiano hafifu wa mikimbio.

Tanzania ilishika nafasi ya nne na pointi 10 baada ya kushinda mechi tano na kupoteza tatu.

Nigeria imemaliza ya tano ikiwa na pointi 10, lakini ilishindwa na Tanzania kwa uwiano wa mikimbio.

Nafasi ya sita ilishikwa na Brazil yenye pointi nane ikiwa juu ya Malawi iliyoshika nafasi ya saba na pointi mbili, huku Sierra Leone ya nane na Cameroon ilimaliza ya tisa ikiwa na pointi moja.