Ndumbaro kuongoza mastaa 200 gofu Arusha

Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kisiga (wa pili kushoto) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Uwanja wa Gofu wa Lugalo leo Novemba 13, 2024 jijini Dar es Salaam. (Kulia kwenda kushoto) Suleiman Rashid, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo AutoMark; Henry Mwanyika, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uwezeshaji Vodacom Business na Hildegard Mung'ong'o, Meneja Mwandamizi wa benki ya NMB.
Dar es Salaam. Zaidi ya wachezaji gofu 200 kutoka nchi mbalimbali za Afrika watashiriki katika mashindano ya Tanzania Open yaliyopangwa kuanza Novemba 21 mpaka 24 kwentye uwanja wa Kili Golf wa Arusha.
Mwenyekiti wa chama cha gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga alizitaja nchi hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Afrika Kusini na wenyeji, Tanzania.
Amesema kuwa wachezaji nyota wa wa Tanzania kama Isihaka Daudi, Ali Mcharo pamoja na Waziri wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro.
Pia katika orodha hiyo wapo wachezaji nyota wa Kenya, John Kibet, Carl Wambasi Makokha, Ndegwa Nderitu, Paul Chidale, Hussein Bagalana (Malawi), Hussein Bagalana (Uganda), Tongoona Charamba (Zimbabwe) na wengine wengi.
Pia wapo wachezaji nyota wanawake kama Vicky Elias, Maryanne Mugo na wengine mbalimbali.
Amesema kuwa mashindano yanachangia pointi kwenye ranki za dunia (WAGR).
"Haya ni mashindano makubwa sana hapa Tanzania na kwa sasa yameingia katika orodha ya viwango ya duniani (WAGR). Tunafuraha kumpata udhamini mkuu, kampuni ya simu ya Vodacom na kuongeza hamasa kwa washiriki,” alisema Kasiga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara, Vodacom Tanzania, Nguvu Kamando, alisema kuwa wameamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la kuinua michezo nchini.
"Vodacom inajivunia kushirikiana na TGU kama mdhamini mkuu wa mashindano ya ‘Vodacom Tanzania Open 2024’," amesema Kamando.