Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nathaniel Chilambo amtega Mnoga Stars

CHILAMBO Pict

Muktasari:

  • Kati ya nyota hao yupo beki wa kulia, Haji Mnoga anayekipiga Patro Eisden ya Ubelgiji ambaye ameitwa kwa mara nyingine kwenye kikosi cha kocha huyo ambacho Septemba 23, 2026 Taifa Stars itakabiliana na Guinea Ikweta na Septemba 27, 2026 itakabiliana na Madagascar, mechi zote zikiwa ni za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Miguel Gmaondi ameita kikosi cha wachezaji 41 watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbili za kuwania kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Guinea Ikweta na Madagascar na ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Ghana, mwezi huu.

Kati ya nyota hao yupo beki wa kulia, Haji Mnoga anayekipiga Patro Eisden ya Ubelgiji ambaye ameitwa kwa mara nyingine kwenye kikosi cha kocha huyo ambacho Septemba 23, 2026 Taifa Stars itakabiliana na Guinea Ikweta na Septemba 27, 2026 itakabiliana na Madagascar, mechi zote zikiwa ni za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Sasa achana na kikosi hicho, Mnoga anaitwa kwa mara nyingine na safari hii kwenye nafasi yake anakutana na beki mpya wa Simba, Nathaniel Chilambo ambaye ameanza vizuri kikosini hapo.

CHILA 01

Kabla ya nahodha wa Simba, Shomari Kapombe kuumia, Mnoga hakuwa anapata nafasi moja kwa moja timu ya taifa na ameitwa kwa mara nyingine ikiwa tayari Chilambo amewaka.

Tangu ajiunge na chama hilo  msimu huu akitokea Salford City ya England, Mnoga alicheza dakika 346 kati ya 360 mechi zote nne. Alianza kwa dakika 90 dhidi ya Anderlecht U23, dakika 90 dhidi ya Lierse, dakika 90 dhidi ya Club Brugge U23 na dakika 76 dhidi ya Beerschot VA.

Msimu uliopita akiwa Salford City, alicheza mechi 32 katika mashindano yote, kwa dakika 2,268 akiwa sehemu ya kikosi kilichoipeleka timu hiyo hatua ya play-off za kupanda daraja.

Anakutana na Chilambo wa Ligi Kuu Bara ambaye amekuwa wa moto, je, Mnoga atapata nafasi ya kucheza mechi hizo mbele ya kitasa hicho cha Simba ambacho kimeanza mechi nne za ligi akicheza kwa nafasi tofauti hadi kiungo.

CHILA 02
CHILA 02

Beki huyo mara ya mwisho kupata nafasi alicheza dakika 72 dhidi ya Morocco kwenye mechi ya AFCON na Tanzania ilipoteza kwa bao 1-0

Chilambo mara ya mwisho kucheza Taifa Stars ilikuwa Septemba 10 kwenye mashindano ya kufuzu AFCON na beki huyo akiwa benchi dhidi ya Guinea, Tanzania ilishinda kwa mabao 2-1.