Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi ang’oa watano Yanga

Muktasari:

YANGA imetamka kwamba haijaridhishwa na hatua ya kukataliwa kwa bao lao dhidi ya Namungo lakini imeweka wazi mipango ya kocha wao Nesreddine Nabi kwa ajili ya msimu ujao.

YANGA imetamka kwamba haijaridhishwa na hatua ya kukataliwa kwa bao lao dhidi ya Namungo lakini imeweka wazi mipango ya kocha wao Nesreddine Nabi kwa ajili ya msimu ujao.

Nabi amewelea mabosi wake kwamba hata kama wanaonewa kwa bao lililokataliwa dhidi ya Namungo lakini ametaka maboresho makubwa katika eneo la ushambuliaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinius ‘Baba Paroko’ ameliambia Mwanaspoti kuwa Nabi anapanga kusajili wachezaji wasiopungua watano katika safu ya ushambuliaji.

“Tunayaona ambayo yanaendelea hatufurahishwi nayo, haiku-wa sare ambayo tulistahili (dhidi ya Namungo) timu inafunga bao halali lakini unaambiwa sio bao,” alisema Albinius.

“Hata hivyo, kama klabu tunajua wapi pa kuanzia kwa msimu ujao na bahati nzuri ni kwamba kumleta kocha mapema (Nabi) kumeanza kuleta matunda kwa kocha kuanza kuonyesha anachotaka kwa msimu ujao.

“Mpaka sasa ripoti ya awali ambayo Nabi ametueleza anataka kuongeza mpaka wachezaji watano katika eneo la ushambuliaji na wengine kuwapisha wapya.”

Akifafanua zaidi Albinius alisema eneo hilo la ushambuliaji ndio litasimamiwa kwa umakini mkubwa ambapo washambuliaji wa kati mawinga na viungo wa pembeni wataongezwa.

“Kocha anasema timu inatengeneza nafasi shida ipo katika kuzitumia kwahiyo lazima tuongeze watu wenye ubora zaidi.

“Huku kwingine kwa viungo wa pembeni nako anataka mtu mwenye ubora zaidi, kwasasa kama tunamkosa Kisinda (Tuisila) hakuna nguvu nyingine pia anataka mtu eneo hilo,” alisema.

Aidha, alisema pia wanakusudia kutafuta kiungo mchezeshaji wa kati ambaye ataongeza ubunifu zaidi wa kutengeneza nafasi.

“Eneo la kiungo ushambuliaji wa kati nako kuna mtu anahitajika kocha anaona hakuna ubunifu wa kutengeneza nafasi nako tutatafuta mtu muafaka atakayekuwa na ubora wa kutengeneza nafasi eneo hilo.”