Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakinyo aporomoka Afrika, kumaliza kifungo Oktoba 18

Wakati Bodi ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Nchini Uingereza (BBBC) ikitaja Oktoba 18 itakuwa siku mwisho ya kifungo cha Hassan Mwakinyo kutocheza ngumi nchini humo, bondia huyo namba moja nchini ameporomoka kwa nafasi moja katika viwango vya ndondi Afrika.

Mwakinyo ambaye tangu 2018 alikuwa ni kinara kwenye uzani wake kabla ya karibuni kuporoka hadi nafasi ya pili, wiki hii ameporomoka tena hadi nafasi ya tatu kwenye uzani wa super welter.

Mabondia wenye upinzani nchini Afrika Kusini,  Roarke Knapp na Brandon Thysse ndiyo wamemporomosha Mwakinyo kileleni kwenye ubora wa uzani wa super welter Afrika.

Knapp sasa ndiye namba moja na Thysse akikamata nafasi ya pili wote wakiwa na nyota tatu na nusu sawa na Mwakinyo aliyetajwa kwenye nafasi ya tatu wakitofautiana pointi.

Mkongo, Emmany Kalombo ni wa nne na Shervantaigh Koopman wa Afrika Kusini anahitimisha tano bora katika uzani wa super welter Afrika.

Kidunia, Mwakinyo amesalia kuwa wa 43 kati ya mabondia 1960 wakati nchini akizidi kuwa kinara kwenye kila uzani 'pound for pound'.

Katika hatua nyingine, BBBC imetaja Oktoba 18 itakuwa ni siku ya mwisho ya bondia huyo kufungiwa kuzichapa nchini humo baada ya kumfungia siku chachee baada ya pambano na Liam Smith la Septemba 3.

Katika pambano hilo, Mwakinyo alipigwa kwa TKO dakika ya 1:46 ya raudi ya nne, kabla ya mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec) kueleza bondia huyo kufungiwa kuzichapa nchini humo.

Tayari BBBC imetaja kupitia Boxrec kwamba Oktoba 18 itakuwa mwisho wa 'kibano' hicho kwa Mwakinyo ambaye siku chache baada ya kufungiwa alisema kimetokana na sheria za nchi hiyo kwa bondia aliyepigwa KO au TKO.

s.Watanzania wengine walioingia 20 bora ya Afrika kwenye uzani huo ni Meshack Mwankemwa aliyetajwa kwenye nafasi ya 15 ya Mfaume Mfaume aliyekwenye nafasi ya 16.