Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtihani mwingine wa Lwandamina kwa Ruvu

Dar es Salaam. Baada ya kukusanya pointi tatu katika mechi tano mfululizo, Azam itakuwa nyumbani kuikabili Ruvu Shooting huku kocha mkuu, George Lwandamina akipiga hesabu za mbali sawa na ilivyo kwa Fredrick Mwasombola wa Mwadui, ambaye atakuwa nyumbani kuikaribisha Polisi Tanzania.

Azam itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Azam Complex kuikabili Ruvu Shooting, kuanzia saa 1 usiku.

Mchezo huo ni mgumu kwa timu zote mbili hasa Azam, ambayo licha ya kuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 28, tangu Novemba 21 haijawahi kuonja ladha ya ushindi kwenye mechi tano zilizopita.

Katika mechi hizo za nyumbani na ugenini, Azam imepoteza pointi 12 na kuvuna tatu baada ya kuambulia sare mfululizo dhidi ya Biashara United 1-1, suluhu na Gwambina mechi zote akicheza ugenini na sare ya 2-2 na Namungo nyumbani.

Azam imefungwa na Yanga bao 1-0 na kipigo kama hicho dhidi ya KMC nyumbani na ugenini.

“Tunahitaji pointi tatu, huo ndiyo mpango wa kila mmoja wetu kwenye timu kesho (leo), alisema kocha George Lwandamina.

Kocha wa Ruvu, Charles Mkwasa alisisitiza kuwa wamejiandaa kuchukua pointi tatu ili kuendelea kujiimarisha kwenye nafasi ya nne katika msimamo.

Kama watashinda watafikisha pointi 27 na kuendelea kusalia kwenye nafasi ya nne huku akihitaji pointi moja kuzifikia 28 za Azam, ambayo ni ya tatu kwenye msimamo.

“Tuko vizuri, tutaikabili Azam kwa tahadhari, lakini kwa mikakati ya ubingwa, vijana wana ari na morali ya ushindi, bila shaka tutachukua pointi tatu,” alisema Mkwasa.

Kwenye Uwanja wa Mwadui, wenyeji Mwadui FC watakuwa na kibarua cha kujinasua mkiani mbele ya Polisi Tanzania, ambayo katika mechi tano za mwisho imevuna pointi sita kwa kushinda moja, sare tatu na kufungwa mechi moja.

Mwadui itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mechi zote tano za karibuni ikiwamo ya mwisho ilipochapwa nyumbani mabao 5-0 na Yanga.

Kocha msaidizi, Fredrick Masombola ambaye ndiye ameachiwa timu baada ya kuachana na kocha mkuu, Khalid Adam hivi karibuni alisema licha ya matokeo mabovu ambayo wamepata mfululizo, bado wanaamini mechi ya leo itafufua matumaini.

Mbeya City yenye pointi 12 itakuwa ugenini kuikabili Biashara ambayo ni ya nane.