Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshambuliaji Kigamboni United aiota Ligi Kuu Bara

KIGAMBONI

Muktasari:

  • Nyota huyo amejiunga na Kigamboni United msimu huu wa 2026-2027, akitokea Coastal United ya jijini, Tanga aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la Januari 21, 2026, baada ya kuachana na maafande wa Tanzania Prisons kutokea jijini, Mbeya.

MSHAMBULIAJI wa Kigamboni United zamani B19 FC, Abdulkarim Segeja amesema licha ya kusaini mkataba wa miezi sita na kikosi hicho, ila atahakikisha anapigania malengo ya timu hiyo kwa msimu wa 2026-2027, ili kuongeza ushindani zaidi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Segeja amesema lengo la kusaini mkataba wa muda mfupi na timu hiyo ni kwa ajili ya kujipanga upya ili arejee tena kucheza Ligi Kuu Bara, ingawa atahakikisha anakipigania kikosi hicho kwa miezi sita atakayoichezea.

“Hii ni nafasi nzuri kwangu ya kuendelea kuonyesha kiwango kizuri, kusaini mkataba wa miezi sita haina maana hatuwezi kukaa chini na kuongeza mwingine zaidi, isipokuwa malengo yangu ni kurudi kucheza tena Ligi Kuu Bara,” amesema Segeja.

Nyota huyo amejiunga na Kigamboni United msimu huu wa 2026-2027, akitokea Coastal United ya jijini, Tanga aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la Januari 21, 2026, baada ya kuachana na maafande wa Tanzania Prisons kutokea jijini, Mbeya.