Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manqoba aachiwa msala Yanga

KOCHA Pict


YANGA jana ilianza maisha mapya chini ya kocha Manqoba Mngqithi ambaye alisimamia mazoezi ya kwanza kikosini hapo tangu kutangazwa kuwa kocha mkuu. Sasa kuna usajili amechiwa ili kuleta mtu sahihi.


Jana Yanga ilianza mazoezi pale Avic Town, siku ya kwanza kwa Mngqithi ndani ya kambi hiyo lakini kuna kazi moja alikabidhiwa siku moja kabla kwenye kikao na mabosi wa juu wa klabu hiyo.


Kwenye kikao cha Mngqithi na mabosi wa juu wa Yanga akiwepo Rais wa klabu hiyo, Hersi Said, kocha huyo raia wa Afrika Kusini aliachiwa jukumu gumu la kutafuta kiungo mkabaji wa maana.

Hata hivyo, Yanga ni kama imemtega Mngqithi ikimtaka kama akipata kiungo huyo kitafanyika kikao cha uamuzi kupima ubora wa kiungo huyo kabla ya kupewa mkataba.

"Tumempa nafasi kocha tumemwambia namna mahitaji yetu yalivyo juu ya kiungo mkabaji labda anaweza kuwa na chaguo sahihi kwenye wachezaji anaowajua," amesema bosi huyo.

KOCH 01

"Tumemwambia atafute na sisi tunaendelea kutafuta, upande mmoja atakaopata lolote tutakaa na kupima kisha kufanya uamuzi wa mwisho kwa kukubaliana kwa pande zote."

Yanga inahaha kutafuta kiungo mkabaji wa kigeni ambapo bado usajili huo unawapasua vichwa mabosi wa klabu hiyo.

Mapema Yanga wiki hii ikapokea taarifa mbaya baada ya kiungo Adolf Mtasingwa aliyekuwa Azam, kusajiliwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakati mabingwa hao wa soka Tanzania wakiwa wanampigia hesabu.

"Unajua Azam wametufanyia ukatili mwingine, walijua kwamba tunamuhitaji Adolf lakini wakaona ni bora kumpeleka mbali kuliko kuja hapa, kwahiyo tunaendelea kutafuta kiungo mwingine," amesema bosi huyo wa juu wa Yanga.

KOCH 02

Yanga pia ilikuwa inataka kumsajili Alphonce Mabula ambaye kwasasa ni mchezaji huru lakini hata hivyo dili hilo limeingiwa na ugumu kutokana na dau kubwa ambalo kiungo huyo amelihitaji.

Tangu kuondoka kwa Khalid Aucho mwishoni mwa msimu wa 2024-2025, Yanga inahaha kutafuta mtu sahihi wa eneo hilo, ambapo viungo wawili wameonekana kushindwa, wakiwemo Moussa Bala Conte na Mohammed Damaro.

Wakati Manqoba akiachiwa msala huo, taarifa zinabainisha kwamba, Yanga imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mkabaji raia wa Nigeria, Morice Chukwu kutoka Singida Black Stars.

KOCH 03

Kiungo huyo aliyetua kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Tanzania msimu wa 2023-2024 akitokea Rivers United ya kwao Nigeria, amezichezea klabu kadhaa hapa nchini ikiwemo Fountain Gate, Tabora United ambayo sasa ni TRA United na Ihefu iliyobadilishwa jina na kuitwa Singida Black Stars.