Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnada mtandaoni wawapa vicheko Watanzania

LIPO Pict

Muktasari:

  • Hili limedhihirika baada ya washindi wa awamu ya tatu wa mnada mtandaoni kujizolea zawadi ikiwamo mmoja kuondoka na runinga janja inchi 55 pamoja na kifurushi cha internet cha mwaka mzima.

Wakati teknolojia ikizidi kukua, Watanzania wanaendelea kunufaika nayo kwa kutumia mitandao wakiuza na kununua bidhaa zao na kuvuna pesa na zawadi nyingine.

Hili limedhihirika baada ya washindi wa awamu ya tatu wa mnada mtandaoni kujizolea zawadi ikiwamo mmoja kuondoka na runinga janja inchi 55 pamoja na kifurushi cha internet cha mwaka mzima.

Mnada huo unaoendeshwa na jukwaa la kidijitali la PIKU Afrika, pia lilishuhudia washindi wengine wawili wakijizolea bidhaa kama pafyumu, vidani vya mkononi na saa ya kisasa huku mwingine akijishindia simu janja.

Jackson Ngonji ndiye aliyeibuka kinara akiondoka na runinga hiyo kutoka kampuni ya LG, huku Jonathan Paul akipata pafyumu, vidani vya mkononi na saa ya kisasa na Niovita Shayo ikikabidhiwa simu janja ya Samsung na spika ya bluetooth.

Washindi hao wanaungana na wengine sita wa mwanzo na kufikia tisa na  Meneja wa Habari na Mawasiliano wa jukwaa hilo, Barnabas Mbunda, amesema ni mafanikio makubwa kuona zaidi ya washindi tisa wamejinyakulia zawadi mbalimbali kwa kushiriki mnada kwa njia ya kidijitali.

Amesema hiyo kwao jukwaa hilo ni fahari kwani washindi katika minada yao wamepata bidhaa  zao bila kikwazo, hali inayodhihirisha uwazi na ubunifu wa mfumo yao.

Amebainisha zawadi mbalimbali zilitolewa, ikiwamo 'kombo' ya bidhaa kwa bei ya chini na ya kipekee. Pia ameeleza bidhaa zote za kielektroniki ambazo washindi wamepata tayari zimekatiwa bima ya mwaka mzima, hivyo washiriki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu usalama au uimara wa bidhaa hizo.

Mbunda aliongeza, promosheni inaendelea na minada mikubwa zaidi bado iko mbele na zawadi kuu kwa sasa ni gari aina ya Toyota Raum ikiwa ni zawadi ya funga mwaka.

“Gari hiyo itatolewa pamoja na mafuta lita 100 kila mwezi kwa mwaka mzima, matengenezo ya bure kwa mwaka, bima kamili ya mwaka mzima. Pia itatolewa pikipiki mpya aina ya TVS, itakayokabidhiwa ikiwa na helmeti na reflector, kadi ya mafuta lita 30 kwa kila mwezi kwa mwaka mzima na bima ya mwaka mzima,” amesema.

Amesema tiketi za mnada kwa wale wanaotaka kushiriki, zinapatikana kwa Sh1,000 tiketi 10, Sh5,000 tiketi 50, Sh10,000 tiketi 100 na Sh100,000 tiketi 1,000.

Mbunda alisisitiza kadri idadi ya tiketi inavyoongezeka, ndivyo nafasi ya kushinda inavyokuwa kubwa zaidi.

Kwa upande wake, Jakson Ngonji, mshindi wa kwanza wa televisheni janja ya inchi 55, ameeleza kwa furaha namna alivyoshinda zawadi hiyo kubwa kwa kutumia dau dogo katika mfumo wa mnada huo wa kidijitali.

“Nilishiriki kwa matumaini na kwa kweli siamini hadi leo. Nawahamasisha vijana na Watanzania kwa jumla wajitokeze kushiriki katika minada hii. Ni fursa ya kipekee kupata bidhaa za thamani kubwa kwa gharama ndogo,” amesema Ngonji.

Jukwaa hilo limeendelea kuwa kinara katika mapinduzi ya minada ya mtandaoni, ikiwapa Watanzania fursa ya kupata bidhaa bora kwa bei nafuu katika mfumo wa kidijitali, wa uwazi na wa kipekee.