Mkwasa: Yanga itakaa sawa baada ya Uchaguzi
Muktasari:
- Alisema klabu hiyo ambayo inapitia katika mtikisiko wa uchumi, itakapokuwa na uongozi kila kitu kitakwenda sawa.
WAKATI wanachama wa Yanga wakisalia na siku 16 kabla ya kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema uchaguzi huo utaiondoa klabu kwenye mtikisiko wa uchumi.
Mkwasa alisema, Yanga iliyumba kutokana na kutokuwa na viongozi kwa muda mrefu ambao wangeweza kuweka mipango kwaajili ya maendeleo ya timu yao.
“Wakati naingia Yanga kama Katibu Mkuu, nilifanya kazi na Mwenyekiti (Yusuf Manji) kwa siku tano tu akawa ameingia kwenye matatizo,”
“Tumekaa muda mrefu bila mwenyekiti, tulipambana, hadi pale tulipofikia,” alisema Mkwasa.
Alisema klabu hiyo ambayo inapitia katika mtikisiko wa uchumi, itakapokuwa na uongozi kila kitu kitakwenda sawa.
Yanga itafanya uchaguzi Mei 5 jijini Dar es Salaam kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao walijiuzuru kwa nyakati tofauti.