Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Minziro: Watu wanataka kunichonganisha na Karia

Kocha wa Geita Gold FC, Fred Minziro akipokea tuzo ya kocha bora wa Ligi Daraja la Kwanza 2020/21 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. PICHA NA LOVENESS BERNARD

Wakati Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia akieleza kwamba hajui aliyerusha video ikimuonyesha amekwepa kusalimiana na kocha wa Geita Gold, Fred Minziro,  amesema video hiyo imetengenezwa kwa lengo la kumchonganisha na kiongozi huyo wa soka nchini.

Baada ya mechi yao ya fainali ya kusaka bingwa wa FDL kati ya Geita Gold na Mbeya Kwanza jana Jumapili jijini Dar es Salaam, Minziro alitajwa kuwa kocha bora wa Ligi hiyo na wakati akielekea kuchukua tuzo yake ndipo video ikaonyesha Karia anakwepa kumpa mkono wa pongezi Minziro.


Karia nje ya tukio hilo ameiambia MCL Digital kwamba haina ukweli na imetengenezwa kwa nia ovu.

"Sijui aliyeiposti alikuwa na maana gani, muulize Minziro atakueleza ukweli," amesema Karia.

Minziro alipoulizwa alisema ni video ambayo imetengenezwa kwa nia ovu ya kumchonganisha na Karia.

"Hivi Karia akatae kunipa mkono kwa sababu gani? ukiachana tu na kuwa rais wa mpira ni rafiki yangu na sijawahi kutofautiana naye, ni watu tu wameamua kuitengeneza kwa nia ovu ya kunichonganisha naye," amesema.

Amesema alipokuwa jukwaani jana, Karia alimwambia ageuke ili apigwe picha na waandishi wa habari.

"Kama angekuwa ananichukia angeniambia hivyo?," alihoji Minziro na kubainisha kwamba hata leo asubuhi ameongea na Karia.

"Sina ugomvi na Karia, ni rafiki yangu tangu nacheza mpira na hata leo asubuhi nimezungumza naye, ni watu tu wanatengeneza vitu vya ajabu ajabu ili kuchonganisha wengine," amesema.

Amesema kama kuna mtu amemsema vibaya Karia baada ya kuangalia video ile basi amemuonea, kwa kuwa ni video ambayo anadai imetengenezwa ili ionekane Karia hakumpa mkono wakati si kweli.