Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgosi ana rekodi Simba Queens

MGOSI Pict

Muktasari:

  • Simba Queens hivi karibuni ilinyakua taji la ligi kuu ikiwa la tano tangu ligi hiyo ianzishwe mwaka 2017.

WAKATI pongezi nyingi zikielekezwa kwa Simba Queens baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu huu, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’ naye ana rekodi zake.

Simba Queens hivi karibuni ilinyakua taji la ligi kuu ikiwa la tano tangu ligi hiyo ianzishwe mwaka 2017.

Kocha huyo, ambaye amekuwa sehemu ya benchi la ufundi la Simba Queens kwa miaka kadhaa, sasa ameongeza taji lake la nne la ligi akiwa ndani ya benchi la timu hiyo, rekodi inayomweka miongoni mwa makocha wenye mafanikio makubwa katika soka la wanawake nchini.

Mbali na viongozi wa klabu, benchi la ufundi Mgosi anastahili sifa kwa namna alivyoweza kuwaunganisha wachezaji wapya na wale waliokuwepo, jambo lililojenga kikosi chenye mshikamano na ushindani mkubwa katika msimu mzima.

Katika baadhi ya mechi ngumu, hasa zile za ugenini mikoani, Simba Queens ilicheza kwa mbinu maalumu za kutafuta pointi tatu. Uwezo huo wa kusoma mazingira ya mchezo ulikuwa sehemu ya silaha iliyowapa ubingwa.

MGO 01

MAFANIKIO

Mgosi alianza kuandika historia yake na Simba Queens msimu wa 2019/20, alipokuwa sehemu ya benchi la ufundi lililoiongoza timu kutwaa ubingwa wa ligi.

Hakukuishia hapo, kwani msimu uliofuata wa 2020/21 alishuhudia tena Simba Queens ikibeba taji na kuendelea kuthibitisha ubora wake katika soka la wanawake.

Msimu wa 2021/22, Simba Queens ilitwaa ubingwa mwingine, lakini safari hiyo ilikuwa bila Mgosi kuwa sehemu ya benchi la ufundi. Katika kipindi hicho timu ilianza chini ya kocha Hababuu Ally, kabla ya Sebastian Nkoma kupewa jukumu la kuiongoza hadi kutwaa ubingwa.

MGO 03

Baada ya kurejea kwenye benchi la ufundi, Mgosi aliendelea na rekodi yake ya mafanikio. Msimu wa 2023/24, akiwa kocha msaidizi wa Juma Mgunda, alichangia kuirejesha Simba Queens kwenye ushindani mkubwa baada ya wawili hao kupewa jukumu la kuinoa timu kufuatia kuondoka kwa Charles Lukula.

Na ubingwa wa msimu huu umeifanya rekodi yake kuwa ya kipekee zaidi, akifikisha mataji manne akiwa sehemu ya benchi la ufundi la Simba Queens.

MGO 02

MWAMBA HASWA

Kilichomtofautisha Mgosi ni uwezo wake wa kubaki kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Simba Queens licha ya mabadiliko ya makocha wakuu yaliyotokea ndani ya klabu hiyo kwa nyakati tofauti.

Amefanya kazi chini ya viongozi na makocha mbalimbali, lakini mchango wake umeendelea kuonekana kupitia uimara wa kikosi na matokeo yaliyopatikana.

MGO 04

Katika mataji matano ambayo Simba Queens imeyanyakua katika historia yake ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, Mgosi amebeba manne, rekodi inayomfanya kuwa mmoja wa makocha walioweka alama kubwa katika mafanikio ya klabu hiyo na soka la wanawake kwa ujumla.

Akizungumzia rekodi hizo kocha huyo ambaye awali aliwahi kuitumikia Simba amesema “Ni jambo zuri unapofanya kazi na unapata mafanikio binafsi kwangu ni kitu kizuri na watu wanaona na kupongeza unachokifanya.”