Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu aichambua MC Alger, Aziz Ki akishusha presha Yanga

FADLU Pict

Muktasari:

  • Yanga inatarajiwa kuvaana na MC Alger kesho katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya mashindano hayo, ikiwa na dhamira ya kutumia Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kukusanya pointi tatu muhimu.

KOCHA wa Yanga, Fadlu Davids, amesema kikosi chake kimejipanga kutumia faida ya kucheza nyumbani dhidi ya MC Alger ya Algeria, akisisitiza kuwa wanahitaji kuanza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi.

Yanga inatarajiwa kuvaana na MC Alger kesho katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya mashindano hayo, ikiwa na dhamira ya kutumia Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kukusanya pointi tatu muhimu.

Fadlu amesema wanaifahamu heshima ya MC Alger kama mabingwa wa Algeria, lakini pia Yanga inajiheshimu na ina malengo makubwa katika mashindano hayo, ikiwemo kufika fainali.

Amesema pamoja na kuwa na ndoto hizo, kwa sasa wanahitaji kuelekeza nguvu zao kwenye mchezo huo wa kwanza ambao anaamini ni muhimu katika kujenga mwanzo mzuri wa safari yao.

FAD 02

"Tunacheza dhidi ya mabingwa wa Algeria. Tunawaheshimu kama timu, lakini pia tunajiheshimu kama Yanga. Tuna ndoto ya kufika fainali, lakini kwanza tunapaswa kuangalia mchezo unaofuata. Mchezo wa kwanza nyumbani ni muhimu sana na lengo letu ni kupata pointi tatu," amesema Fadlu.

Kocha huyo amefichua kuwa benchi lake la ufundi limefanya uchambuzi wa MC Alger na kubaini kuwa ina wachezaji wenye uwezo na aina tofauti za uchezaji katika nafasi mbalimbali, jambo linalohitaji umakini mkubwa katika kukabiliana nao.

Amesema mabadiliko ya benchi la ufundi la wapinzani hao pia yanafanya mchezo kuwa na changamoto ya ziada, kwani wamekuwa na kocha mpya aliyekiongoza kikosi hicho katika mchezo wake mkubwa wa hivi karibuni dhidi ya Kabylie.

FAD 03

Hata hivyo, Fadlu amesema Yanga haitaki kujikita zaidi katika kuangalia wapinzani pekee, bali itatumia nguvu zake katika kutekeleza falsafa yake ya soka la kushambulia.
Amesema wanataka kutawala mchezo na kuilazimisha MC Alger kucheza kwa namna ambayo Yanga itakuwa imeipangia huku wakiepuka kuacha nafasi zitakazotumiwa na wapinzani katika mashambulizi ya kushtukiza.

"Ni muhimu tunapokuwa tunashambulia tusijisahau katika ulinzi. MC Alger wanaweza kuwa hatari sana katika mashambulizi ya kushtukiza. Tukiwapa nafasi hizo wanaweza kuzitumia kutuumiza," amesema.

Fadlu ameongeza kuwa ushindi katika mchezo wa kwanza ni muhimu, akieleza kuwa MC Alger inaweza kuridhika na sare ugenini na kutumia mbinu za kupunguza kasi ya mchezo endapo itapata matokeo inayoyahitaji.

Kocha huyo pia amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuwa sehemu ya nguvu ya kikosi chake, akiamini mazingira yatakayoundwa na mashabiki yanaweza kuwapa wachezaji msukumo wa kupambana hadi mwisho.

FAD 01

Kwa upande wake, kiungo wa Yanga, Aziz Ki, amesema kikosi hicho hakina presha kuelekea mchezo huo, akieleza kuwa wachezaji wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuanza kwa mashindano hayo.

Azizi Ki amesema maandalizi waliyoyafanya yanawapa nafasi ya kuingia uwanjani wakiwa na furaha na kuonyesha kile walichokifanyia kazi badala ya kuwa na presha ya  matokeo.

"Kwetu hakuna presha. Tumekuwa tukifanya kazi kila siku na sasa siku ya mchezo imefika. Tunapaswa kufurahia wakati huu kwa sababu tumekuwa tukisubiri kwa hamu muda huu ufike," amesema Azizi Ki.