Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbili kupigwa leo Ligi Kuu Bara

LIGI Pict

Muktasari:

  • Polisi ilianza ligi kwa kasi nzuri ikitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam, kisha kushinda mechi mbili lakini ikapata shida hivi karibuni, ikifungwa dhidi ya Singida Black Stars na Coastal Union.

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo Jumamosi kwa mechi mbili kuchezwa ambapo Polisi Tanzania itaikaribisha Mbeya City, huku Coastal Union ikiwa mwenyeji wa JKT Tanzania.

Pale Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Polisi Tanzania itakuwa na dakika 90 zingine za kubadilisha matokeo baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo zilizopita.

Polisi ilianza ligi kwa kasi nzuri ikitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam, kisha kushinda mechi mbili lakini ikapata shida hivi karibuni, ikifungwa dhidi ya Singida Black Stars na Coastal Union.

Kocha wa Polisi Tanzania Mbwana Makata, akizungumzia mchezo huo amesema: “Nikweli hatujafanya vizuri kwenye mechi zilizopita ingawa tulicheza vizuri kidogo, tumeyafanyia kazi mapungufu ambayo tuliyaona, tunataka kushinda kesho (leo) ili turudishe mwendo wetu mzuri.”

LIG 03

Mbeya City ni kama imeanza kujipata, baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu, ikashinda tatu na kutoa sare moja ya mwisho dhidi ya TRA United.

Kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga, amesema: “Tunakwenda kucheza mchezo wa pili mfululizo ugenini, tunakutana na timu nzuri ambayo inataka kupata matokeo mazuri nyumbani, tumejipanga na ugumu huo.”

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, Polisi Tanzania ina nafasi ya kurekebisha pale ilipokosea mechi mbili zilizopita, huku Mbeya City ikisaka ushindi wa ugenini baada ya kutoka suluhu na TRA United uwanjani hapo.

LIG 02

Saa 1:00 usiku, Coastal Union itakuwa nyumbani ikitokea ugenini ilipoichapa Polisi Tanzania, ikiikaribisha JKT Tanzania.

Coastal inataka kushinda mechi yake ya pili msimu huu ambapo kocha wa kikosi hicho, Fikiri Elias akizungumzia mchezo huo amesema: “Wote tunafahamu kwamba JKT Tanzania ni timu nzuri, inafundishwa na kocha mzuri, tutakuwa nyumbani, tumejipanga kutafuta ushindi wetu mwingine itakuwa mechi ngumu kwa timu zote.” JKT yenyewe haina mwendo mbaya kwa sasa baada ya kuanza msimu kichovu, ikiangusha pointi nane kwenye mechi zake tatu za kwanza ikajipata na kuanza kushinda mechi mbili za mwisho.

Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo huku akikiri kwamba wenyeji wao huwa wanawapa mechi ngumu.

LIG 01

“Mechi zote ni ngumu lakini kuna ugumu kwetu tunapokutana na Coastal Union ikiwa kwao, maandalizi yetu yamekwenda vizuri, tupo tayari kwa mchezo.”

JKT Tanzania katika mechi tano ilizocheza msimu huu, haina matokeo mazuri sana ikikusanya pointi saba kufuatia kushinda mbili sawa na ilizopoteza, huku sare ikiwa moja.

LIG 04

Coastal Union yenyewe ndiyo hali mbaya zaidi kwani mechi tano ilizocheza, imekusanya pointi nne, ina sare moja sawa na ushindi ilioupata huku ikipokea vichapo vitatu.