Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbadala wa Okwi, Bocco gumzo Simba

WINGA wa zamani wa Simba, Mnenge Suluja amekiangalia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kisha akatamka maneno mazito.

Amesema Simba haiwezi kupambana kama hakutaletwa mastraika matata ili kuwa mbadala wa washambuliaji Emmanuel Okwi na John Bocco, ambao wamekinukisha kinoma msimu huu.

Suluja amesema ameifuatilia Simba kwa makini kwenye mechi zake za Ligi Kuu na amegundua pacha hao wanapokesana kikosi basi huwa ni majanga na timu inapwaya.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, Suluja alisema usajili ujao wa Simba, mabosi wanapaswwa kutuliza akili na kusajili washambuliaji makini na wanaojua kupasia nyavuni ili kuipa makali zaidi timu yake hiyo.

Alisema Okwi na Bocco wakikosekana timu hiyo inakuwa inayumba kwa kuwa, hakuna mbadala jambo ambalo limeonekana wazi katika mechi ambazo nyota hao wawili hawapo.

“Unaona pale kwenye ushambuliaji akikosekana Bocco au Okwi basi timu inakuwa haiko sawa katika kufunga, sasa inatakiwa wasajili washambuliaji mbadala ambao ni wazoefu na wanaolijua goli,” alisema Suluja.

Hata hivyo, winga huyo aliwapongeza nyota wa Simba kwa kuweza kunyakuwa ubingwa huo na amesema kilichobaki sasa wajipange kwa ajili ya michuano mikubwa ya Afrika na watashiriki katika Klabu Bingwa Afrika mwakani.

“Kwanza niwapongeze kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kazi bado haijaisha wanatakiwa sasa kujiandaa mapema kwa mashindano ya kimataifa ili nako wafanye vyema,” aliongeza.