Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele amkosha kocha Mholanzi

Muktasari:

  • Mayele alifunga bao moja juzi katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Kagera Sugar na kumfanya nyota huyo kufikisha mabao 16 msimu huu akiifikia rekodi aliyoiweka msimu uliopita nyuma ya aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole aliyefunga 17.

KOCHA Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Van Der Pluijm amesema licha ya kubakia michezo minne ili msimu kuisha ila kwake binafsi hadi sasa mchezaji bora ni mshambuliaji na kinara wa ufungaji bora Ligi Kuu Bara nyota wa Yanga, Fiston Mayele.

Mayele alifunga bao moja juzi katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Kagera Sugar na kumfanya nyota huyo kufikisha mabao 16 msimu huu akiifikia rekodi aliyoiweka msimu uliopita nyuma ya aliyekuwa mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole aliyefunga 17.

Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm alisema wapo wachezaji wengi ambao wamefanya vizuri ila Mayele ameonyesha utofauti mkubwa.

"Kuona mchezaji anafunga mabao 15 na kuendelea kwa misimu miwili mfululizo sio jambo la kawaida na wengi wamekuwa hawana hicho kiwango. Ana spidi, anajua jinsi ya kujipanga, utulivu wake mbele ya lango la mpinzani na ni mmaliziaji mzuri."

Pluijm aliongeza kitu kingine kinachomtofautisha nyota huyo na wengine ni kutokuwa na majivuno kwani baadhi yao wakiona wamefanikiwa hujisahau jambo linalowafanya kuzorotesha vipaji vyao pindi tu wanapoyazoea mazingira ya sehemu husika.

Wakati Pluijm akiongea hayo ila Mayele ana kazi kubwa ya kufanya katika michezo mitano iliyobaki kwa Yanga kwani kati ya hiyo ni timu mbili tu ambazo hajazifunga ikiweno Simba anayoenda kukutana nayo Jumapili hii na mchezo wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika michezo iliyobaki kwa Yanga mbali na hiyo ni dhidi ya Singida Big Stars ambao tayari mchezo wa kwanza ameifunga mabao matatu (Hat-Trick) huku Dodoma Jiji na Mbeya City kila mojawapo akiwa ameifunga mawili katika mzunguko wa kwanza.