Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maxi apewa Azam FC, Onana kuanza na Singida

Muktasari:

  • Yanga iliyomtambulisha Nickson Kibabage na kuhusishwa kumsainisha Maxi Mpia Nzengeli imepewa Azam kwenye ya ufunguzi wa mechi hizo zilizofanyiwa marekebisho kidogo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoka kuhusisha Bingwa wa Ligi Kuu na yule ya Kombe la ASFC

MKWAKWANI Tanga patachimbika wakati mechi nne za Ngao ya Jamii zitakapaopigwa kuanzia Agosti 9 hadi 13, ambapo mashabiki wa Simba, Yanga, Azam na Singida Big Stars wataanza kuziona mashinie mpya za timu hizo zikiwasha moto uwanjani.

Yanga iliyomtambulisha Nickson Kibabage na kuhusishwa kumsainisha Maxi Mpia Nzengeli imepewa Azam kwenye ya ufunguzi wa mechi hizo zilizofanyiwa marekebisho kidogo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoka kuhusisha Bingwa wa Ligi Kuu na yule ya Kombe la ASFC.

Maxi na Kibabage watakaoanza kazi chini ya kocha mpya, Miguel Angel Gamondi watavaana na Azam yenye Feisal Salum 'Fei Toto', Cheikh Sidibe, Gibril Sillah na Alassane Diao mechi itakyopigwa kuanzia saa 1:00 usiku.

Siku inayofuata itakuwa ni zamu ya Willy Onana, Aubin Kramo na Che Fondoh Malone kuivaa Singida Big Stars wakiwa na uzi wa Simba iliyowasajili na kuwatambulisha mbele ya mashabiki wa klabu hiyo.

Mshindi wa mechi hizo watakutana kwenye fainali itakayopigwa Agosti 13 kuanzia saa 1:00 usiku mara baada ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu utakaozikutanisha timu zitakazopoteza mbele ya wanafainali hao.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ngao ya Jamii kuhusisha timu nne, ikiwa ni kama nusu fainali flani, kwani kwa miaka yote tangu mechi hizo za ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ilikuwa ikihusisha timu mbili tu, awali zilizokuwa zikimaliza nafasi mbili za juu za Ligi Kuu kisha ikaboreshwa kwa kushindanisha bingwa wa Ligi Kuu na mshindi wa FA (sasa ASFC).

Misimu miwili iliyopita, Yanga ilitwaa Ngao kwa kuifunga Simba, ikianza kwa kuichapa bao 1-0 likiwekwa kimiani na Fiston Mayele kisha kupigwa tena 2-1, Mayele akifunga tena na lile la kufutia machozi la Mnyama likiwekwa kimaini na Pape Ousmane Sakho.