Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Wanawake kuendelea Novemba 04

WPL Pict

Muktasari:

  • Katika mechi za ufunguzi zilizochezwa Oktoba 28, mashabiki walishuhudia msisimko wa aina yake baada ya kufungwa kwa mabao 21 katika mechi sita kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania itaendelea tena Novemba 04, ikiwa ni raundi ya pili ya ligi hiyo, baada ya kushuhudia mechi za ufunguzi zenye ushindani mkubwa.

Katika mechi za ufunguzi zilizochezwa Oktoba 28, mashabiki walishuhudia msisimko wa aina yake baada ya kufungwa kwa mabao 21 katika mechi sita kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Raundi hii ya pili ya Novemba 04, inaleta mechi sita za kusisimua huku timu zikiwania kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi. Uwanja wa Ushirika utashuhudia mechi moja na Kilimanjaro Wonders itamenyana na Mashujaa Queens kuanzia saa 10 jioni.

BWAMK 02

Wakati huohuo, Uwanja wa Karume mwenyeji Bunda Girls ataikaribisha JKT Queens, huku Fountain Gate Princess ikiikaribisha Simba Queens Uwanja wa Jamhuri.

Viwanja vingine vitakavyonogesha raundi hii ni pamoja na CCM Samora na Ceasiaa Queens itavaana na Bunda Queens, wakati Tausi FC ikikabiliana na Alliance Girls huko Nyamagana. Vilevile, Geita Queens itakuwa nyumbani katika dimba la Nyankumbu kucheza dhidi ya Yanga Princess.

SIMB 03

Kocha wa Alliance, Sultan Juma amesema tulianza na ushindi dhidi ya Ceasiaa Queens lakini kuna maeneo tumeboresha eneo la umaliziaji.

"Tulifunga mabao 2-0 lakini tulikosa nafasi nyingi ambazo kama tungekuwa makini tungefunga mabao mengi lakini hizi siku nne zilikuwa za maboresho."