Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Wembe achekelea ushindi wa kwanza

WEMBE Pict

Muktasari:

  • Wembe iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fufuni katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa Oktoba 11, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Owen Ngidu dakika ya 56.

KOCHA Mkuu wa Wembe, Ally Manyani amesema walistahili kupata ushindi wa mabao mengi zaidi dhidi ya Fufuni, lakini washambuliaji wake walishindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.

Wembe iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fufuni katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa Oktoba 11, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Owen Ngidu dakika ya 56.

Manyani amesema moja ya kazi kubwa anayoenda kuifanya katika mazoezi ni kuhakikisha washambuliaji wanatumia nafasi wanazopata kufunga mabao badala ya kuzipoteza.

Kocha huyo amesema amefurahishwa na ushindi huo ambao ni wa kwanza kwake tangu ajiunge na Wembe, akichukua nafasi ya Juma Pweka aliyeachana na timu hiyo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Uhamiaji.

Amesema kabla ya ushindi huo, hakuwa amefanikiwa kuiongoza timu hiyo kupata ushindi, hivyo matokeo dhidi ya Fufuni yamempa furaha na kumwongezea hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Manyani alisisitiza wataendelea kufanyia kazi umaliziaji wa nafasi wanazotengeneza ili kuongeza idadi ya mabao katika michezo ijayo.

“Ligi ya Zanzibar ni nzuri kwa sababu ina ushindani mkubwa, hivyo kila mechi inakuwa ngumu. Ndiyo maana ninawaandaa wachezaji wangu vizuri,” amesema.

Wembe imeshinda michezo miwili kati ya saba iliyocheza, tayari imekusanya pointi nane, ikiwa katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo. Ina pointi sawa na Kipanga, iliyopo nafasi ya tisa na Mlandege, inayoshika nafasi ya kumi.

Timu hiyo inatarajiwa kushuka dimbani kesho Jumapili Oktoba 18, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, kuikaribisha Mwenge, ambayo ina pointi tano.