Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC FC Ligi Kuu wanaitaka

KMC

Muktasari:

  • Ikiwa KMC FC itaendelea na mwenendo wake wa sasa na kumaliza msimu wa 2026/27 bila kupoteza mchezo wowote, itaweka rekodi mpya katika historia ya mashindano hayo.

KMC FC imeanza vizuri kampeni zake za Ligi ya Championship msimu wa 2026/27, ikiwa haijapoteza mchezo wowote kati ya tisa iliyocheza. Hata hivyo, pamoja na mwenendo huo mzuri, timu hiyo inakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuendeleza rekodi hiyo hadi mwisho wa msimu.

Miongoni mwa malengo inayoweza kuyaweka ni kumaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote wa Championship, jambo ambalo halijafanikiwa na timu yoyote katika misimu mitatu iliyopita.

KMC, iliyoshuka daraja baada ya kumaliza katika nafasi ya 16 na ya mwisho kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/26 ikiwa na pointi tisa, msimu huu imecheza mechi tisa, ikishinda tano na kutoka sare nne. Matokeo hayo yameifanya kufikisha pointi 19 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Katika msimu wa 2025/26, Geita Gold ndiyo iliyokuwa karibu zaidi na rekodi hiyo baada ya kupoteza mchezo mmoja pekee kati ya 30 iliyocheza.

Msimu wa 2024/25, Mbeya City ilipoteza mechi mbili, huku katika msimu wa 2023/24, KenGold FC, nayo kutoka Mbeya, ikipoteza mechi mbili.

Kwa maana hiyo, tangu msimu wa 2023/24, Geita Gold ndiyo timu iliyokaribia zaidi kumaliza msimu wa Championship bila kupoteza, baada ya kupoteza mchezo mmoja pekee.

Ikiwa KMC FC itaendelea na mwenendo wake wa sasa na kumaliza msimu wa 2026/27 bila kupoteza mchezo wowote, itaweka rekodi mpya katika historia ya mashindano hayo.