Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Yanga Princess aanza kukiwasha Uturuki

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Precious, ambaye ni miongoni mwa viungo wenye uzoefu wa kucheza soka la wanawake Tanzania, amecheza mechi yake ya kwanza kwenye ligi hiyo akiwa tayari amepewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

KIUNGO fundi wa Nigeria, Precious Christopher maarufu kama ameanza kwa kishindo maisha yake mapya kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Uturuki baada ya kuanza katika kikosi cha kwanza na kuisaidia timu yake mpya, Unyekatadin, kupata ushindi wa bao 1-0.

Precious, ambaye ni miongoni mwa viungo wenye uzoefu wa kucheza soka la wanawake Tanzania, amecheza mechi yake ya kwanza kwenye ligi hiyo akiwa tayari amepewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Kiungo huyo hakusubiri muda mrefu kuanza kuonyesha kile kilichowafanya wamsajili, akisaidia timu yake kupata pointi tatu muhimu katika mchezo wake wa kwanza wa msimu.

Meneja wa kiungo huyo aliyewahi kutamba Simba Queens na Yanga Princess, Abiola Babatunde amesema kumpekea Precious ligi ya Uturuki ni miongoni mwa uamuzi bora akiamini hilo linaweza kumsaidia kukuza kiwango chake.

“Ligi ya Uturuki imekuwa sana naamini kwa alivyoanza kuonyesha ubora wake inaweza kumpa nafasi nyingine na kuongeza soko lake najua ni mchezaji mzuri sana na ana uwezo mkubwa,” amesema Babatunde na kuongeza

KIU 01

“Ligi ya Tanzania imemkuza sana kwa sababu ukanda huu wa Afrika ni miongoni mwa ligi bora na naiona ndani ya misimu mitano itakuwa bora zaidi, nafikiri ushindani alioupata Simba na Yanga utamuongezea uzoefu mkubwa.”

Uzoefu huo wa kucheza katika mazingira tofauti ya soka la wanawake umemjengea kiungo huyo uwezo wa kuhimili ushindani, jambo ambalo sasa linamuweka kwenye mtihani mpya wa Ligi Kuu ya Uturuki. Kwa kuanza mchezo wake wa kwanza katika kikosi cha kwanza na timu yake kuondoka na ushindi wa bao 1-0, Precious tayari ameanza safari yake mpya na mguu mzuri.