Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo JKT Queens afichua jambo

JOYCE Pict

Muktasari:

  • Mafanikio hayo yanaifanya JKT Queens kuendelea kuwa na matarajio makubwa katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Kiungo wa JKT Queens, Joyce Lema amesema kucheza katika kikosi hicho ambacho kimejitengenezea jina ndani na nje ya Tanzania kunampa motisha ya kupambana zaidi ili kuendelea kuipigania nembo ya timu hiyo.

Joyce amesema mafanikio ya JKT Queens katika Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa, pamoja na ushindani uliopo katika kikosi, yanawafanya wachezaji kutokubweteka bali kuendelea kujituma katika mazoezi na mechi ili kupata nafasi na kuisaidia timu kufikia malengo yake.

Amesema “Kucheza hapa kunatupa changamoto ya kupambana kwa sababu JKT ni timu kubwa na yenye mafanikio."

JOY 01

JKT Queens ni miongoni mwa timu zenye mafanikio makubwa katika soka la wanawake Tanzania, ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake mara nne huku Simba Queens ikibeba mara tano.

Mbali na mafanikio ya ndani, timu hiyo pia imeandika historia Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya CECAFA mwaka 2023 na 2025, ikiwa timu ya kwanza kushinda taji hilo mara mbili.

JOY 02

Mwaka 2023, JKT Queens ilitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Commercial Bank of Ethiopia kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0, huku mwaka 2025 ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, bao lililowekwa kimiani na Winfrida Gerald.

Mafanikio hayo yanaifanya JKT Queens kuendelea kuwa na matarajio makubwa katika mashindano ya ndani na kimataifa.