Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Namungo, Mbeya City yakimbilia Tukuyu

Muktasari:

  • Kambi hiyo ya takribani siku 10 ikikamilika, Novemba 15, 2026 timu hiyo inatarajia kurejea maskani kwake kufanya maandalizi ya mwisho kuifuata Namungo, mechi itakayopigwa Novemba 20, 2026 mkoani Lindi.

WAKATI Mbeya City ikijiandaa na mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, kikosi hicho kimetimkia Mji wa Tukuyu, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya huku kikiweka matumaini ya kurejea na nguvu mpya.

Kambi hiyo ya takribani siku 10 ikikamilika, Novemba 15, 2026 timu hiyo inatarajia kurejea maskani kwake kufanya maandalizi ya mwisho kuifuata Namungo, mechi itakayopigwa Novemba 20, 2026 mkoani Lindi.

Mbeya City inaifuata Namungo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mechi ya mwisho, huku ikiwa nafasi ya 11 katika msimamo wa LIgi Kuu Bara na pointi 13 baada ya mechi 10, huku wapinzani ni wa saba na pointi 15.

Nahodha wa timu hiyo, Eliud Ambokile alisema matokeo ya mechi iliyopita yaliongeza nguvu, ari na kujiamini katika kujipanga na michezo inayofuata akitoa matumaini matarajio ni kufanya vizuri.

“Tunaendelea kupambana japokuwa ugumu na ushindani ni mkubwa, lakini ushindi wa mechi iliyopita umerejesha nguvu kwa kuwa kabla ya hapo tulipoteza kadhaa, hatujakata tamaa tukiamini kuwa bora,” alisema Ambokile.

Ofisa habari wa timu hiyo, Gwamaka Mwankota alisema wameamua kuweka kambi hiyo Tukuyu kutokana na hali ya hewa na mazingira tulivu akitamba kwa sasa City itampiga yeyote wanayekutana naye.

“Ni mapendekezo ya benchi la ufundi kwakuwa mazingira ya huku ni mazuri kuanzia hali ya hewa, mazingira na utulivu, tunaamini kuanzia mechi dhidi ya Namungo kazi itaonekana uwanjani,” alisema.