Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kindoki: Tulieni mambo mazuri yanakuja

Muktasari:

Kipa Klaus Kindoki alifanya vizuri katika mchezo dhidi ya Namungo wa Kombe la FA akiisaidia Yanga kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe hilo kwa ushindi wa bao 1-0

Dar es Salaam.Kipa wa Yanga, Klaus Kindoki amesema licha ya mashabiki wa soka kumpongeza kwa kucheza vyema katika mchezo dhidi ya Namungo, bado ana safari ndefu ya kurudisha kiwango chake.

Kindoki amesema bado hajaridhika na kiwango chake ambapo anataka kufanya vizuri zaidi kuisaidia klabu yake.

Kipa huyo ambaye hakuanza vyema licha ya kusajiliwa kwa matarajio makubwa amesema kinachomsaidia sasa ni kutokana na kufahamu kuwasiliana na wachezaji wenzake kwa lugha ya kiswahili ambayo kabla ilimpa shida katika kuelewana.

Amesema sasa anawajua mabeki wa Yanga kwa ubora wao na makosa yao ambapo nafasi hiyo imenipa mwanga wa kujua kufanya kipi kuhakikisha hawafungwi.

Amesema kitendo cha mashabiki kumpongeza wakidai alifanya vizuri anataka kutumia morali hiyo kuongeza juhudi mazoezini.

"Watu wanaona nimecheza vizuri inawezekana, lakini mimi binafsi bado nahitaji kuonyesha uwezo zaidi ili niisaidie timu yangu," amesema Kindoki.

"Watu wanaponipongeza wananipa morali ya kujituma zaidi na sio kubweteka, kwasasa jambo linalonisaidia sasa tunawasiliana vyema na wachezaji wenzangu wakati nafika lugha ya kiswahili ilinisumbua."