Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichomng'oa Msemaji KMC

BODI ya Wakurugenzi ya KMC imemwondoa Msemaji wa timu hiyo, Christina Mwagala kwenye nafasi hiyo na kile kilichomng’oa kikiwekwa sirini, huku klabu ikiwa tayari imeanza mchakato wa kusaka msemaji mpya.

Christina aliyekuwa mmoja ya wasemaji wachache wa kike wa timu za Ligi Kuu Bara, amekuwa na timu hiyo kwa zaidi ya misimu mitatu amejikuta kibarua chake kinaota nyasi na hivi sasa uongozi upo kwenye mchakato wa kutafuta msemaji mpya.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo, zinadai kuwa msemaji ingawa mkataba wake ulikuwa umemalizika, lakini kulikuwepo na mchakato wa kumwongeza mkataba mpya lakini imeshindikana kutokana na sababu za ndani ambazo hazikuwekwa wazi.

“Ni kweli hatakuwa miongoni mwa wafanyakazi wetu, mkataba wake umemalizika lakini hiyo haikuwa sababu ya kuachana naye, kuna mambo ambayo ni ya ndani zaidi,” alisema kiongozi huyo.

Mwanaspoti lilipomtafuta Christina alisema kuwa; “Hata mimi nimeona kwenye mitandao ila kama ipo ama itatokea hapo baadaye basi nitazungumzia.”