Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KenGold yapata somo ugenini, yazitaka tisa fasta

Muktasari:

  • Timu hiyo ya wilayani Chunya iliyowahi kucheza Ligi Kuu kwa msimu mmoja 2024-2025 na kushuka daraja, haijawa na matokeo mazuri ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi tisa baada ya mechi tisa.

BAADA ya kuvuna pointi mbili katika mechi sita ilizocheza ugenini, KenGold imeanza kuzipigia hesabu pointi tisa za michezo ijayo nyumbani kwenye Ligi ya Championship.

Timu hiyo ya wilayani Chunya iliyowahi kucheza Ligi Kuu kwa msimu mmoja 2024-2025 na kushuka daraja, haijawa na matokeo mazuri ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi tisa baada ya mechi tisa.

Katika mechi sita nyuma, timu hiyo imecheza moja nyumbani na tano ugenini ikipata sare mbili na kupoteza nne na sasa itakuwa nyumbani wilayani Chunya kuzipokea tatu mfululizo.

Kesho Jumamosi, itaanza shughuli dhidi ya vibonde wa ligi hiyo, TMA ya mkoani Iringa kisha kuwapokea ndugu zao, Tanzania Prisons kabla ya kumaliza na Gunners.

Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Charles Masai alisema licha ya kuwa na ratiba ngumu lakini bado hawajapoteza mwelekeo kwa kuwa mechi tatu zinazofuata nyumbani wakikaza wanarejea nafasi za juu.

Alisema matokeo ya ugenini hayajawa mazuri sana kwao tofauti na matarajio waliyokuwa nayo na msimu huu lolote linawezekana na ndoto zao ni kuirejesha timu Ligi Kuu.

“Ugenini tumeondoka na somo namna ya kupambana nyumbani, tunaahidi mechi tatu zijayo hatutarajii kuacha hata pointi yoyote, hatujapoteza mwelekeo na bado tupo katika hesabu nzito.

“Championship ni ya kutumia nguvu nyingi na hesabu, matarajio yetu ni kuona tunamaliza nafasi mbili za juu na tunayo nia na malengo ya kurejea Ligi Kuu, ushirikiano na kujituma ndivyo vitatupeleka huko,” alisema nyota huyo.