Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze arejea Tanzania akikabidhiwa Kagera Sugar

KAZE Pict

Muktasari:

  • Kaze anarejea Ligi Kuu Tanzania na historia nzuri ya kubeba mataji akiwa Yanga alipofanya kazi na aliyekuwa Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ambao baadaye waliungana tena Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. 

Muda mchache baada ya kuachana na Juma Kaseja, uongozi wa Kagera Sugar umemtambulisha Cedrick Kaze kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo. 

Kaseja ameachana na timu hiyo baada ya kuiongoza katika mechi sita za Ligi Kuu Bara msimu huu akivuna pointi mbili na kuiacha nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo. 

Baada ya makubaliano ya pande mbili, uongozi wa timu hiyo umetangaza kumpa kazi Kaze ambaye anarejea nchini baada ya kuhudumu Yanga akiwa kocha mkuu, baadaye msaidizi akifanya kazi na Mtunisia, Nasreddine Nabi. 

KAZ 01
KAZ 01

Kocha huyo raia wa Burundi kabla ya kutua Kagera Sugar, alikuwa anainoa Kaizer Chief ya Afrika Kusini aliyoachana nayo msimu wa 2025-2026 ulipomalizika. 

Mwenyekiti wa Kagera Sugar, Francis Lubandi, amesema baada ya tathimini waliyoifanya, wamejiridhisha Kaze anaweza kuwafikisha wanapotaka na kuanzia leo ataanza majukumu yake. 

"Tathimini tuliyoifanya na uchunguzi tumeona na kujiridhisha kuwa Kaze anaweza kutusaidia na kutufikisha tunapopataka, mashabiki watuunge mkono kwa kipindi hiki tuweze kurejea upya," amesema kiongozi huyo. 


KAZ 02

Kwa upande wake Kocha Kaze amesema ni furaha kubwa kwake kuwa katika timu hiyo yenye historia katika medani za soka nchini, akieleza kuwa kazi itaanza rasmi kesho Jumanne. 

"Siwezi kuzungumza mengi lakini nachoweza kuahidi kwa wadau na mashabiki wa Kagera Sugar ni kuona timu inaondoka nafasi za chini na kupanda juu," amesema Kaze. 

Kagera Sugar baada ya mapumziko mafupi, inatarajia kurejea kambini kesho Jumanne kuendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, utakaopigwa Oktoba 8, 2026 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.