Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kawempe yafikia rekodi ya Simba CAF

KAWEMPE Pict

Muktasari:

  • Msimu wa 2022, Simba Queens iliweka historia baada ya kufanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo yaliyopigwa nchini Morocco, ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo ya Tanzania kufika hatua hiyo katika historia yake.

REKODI ya Simba Queens katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake iliyodumu kwa miaka minne bila timu nyingine kutoka ukanda wa CECAFA kuivunja, imefikiwa na Kawempe Muslim Ladies ya Uganda ambayo imetinga kucheza nusu fainali baada ya kuitandika USFA Bamako ya Mali kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi B.

Msimu wa 2022, Simba Queens iliweka historia baada ya kufanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo yaliyopigwa nchini Morocco, ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo ya Tanzania kufika hatua hiyo katika historia yake.

Mafanikio hayo yaliifanya Simba kuwa moja ya timu zilizoweka alama katika uwakilishi wa Ukanda wa CECAFA kwenye mashindano hayo ya ngazi ya Afrika.

KAWE 01

Katika kampeni hiyo, Simba ilianza kwa kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji AS FAR Rabat, kabla ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls ya Liberia.

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia katika mchezo wa mwisho wa kundi ndio uliowahakikishia Wanamsimbazi hao kukata tiketi ya kucheza nusu fainali.

Hata hivyo, safari ya Simba iliishia hatua ya nusu fainali baada ya kuondolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ilipotandikwa kwa bao 1-0.

KAWE 02

Tangu wakati huo, hakuna timu nyingine iliyowakilisha ukanda wa CECAFA iliyofanikiwa kufikia hatua hiyo katika mashindano hayo ya CAF, hadi Kawempe ilipofanya hivyo mwaka huu.

Mbali na Kawempe na Simba timu nyingine kutoka CECAFA zilizowahi kushiriki mashindano ya Afrika lakini zikashindwa kuvuka hatua hiyo ni Vihiga Queens ya Kenya (2021), JKT Queens ya Tanzania (2023 na 2025) pamoja na Commercial Bank of Ethiopia (CBE) ya Ethiopia (2024) na zote ziliishia makundi.

Kawempe imefikia mafanikio hayo katika ushiriki wake wa kwanza wa fainali hizo zinazoendelea Misri. Timu hiyo ilianza kwa kishindo baada ya kuichapa AS FAR Rabat mabao 3-2, kabla ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya AMPEM Darkoa ya Ghana, lakini ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya USFA Bamako katika mchezo wa mwisho wa Kundi B ukaihakikishia nafasi ya pili na tiketi ya nusu fainali.

KAWE 03

Katika mchezo huo dhidi ya USFA Bamako, Jovia Nakagolo aliipa Kawempe bao la kwanza dakika ya 40, kabla ya Agnes Nabukenya kufunga mabao mawili kipindi cha pili na kuipa timu hiyo ushindi wa mabao 3-0. Mafanikio hayo yameifanya Kawempe kufikia hatua ambayo Simba Queens iliweka kama alama ya uwakilishi wa CECAFA mwaka 2022.