Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kasi ya miguu yawapa viwanja mabingwa Kili marathoni

Mabingwa wa mbio ya kilomita 42 ya Kilimanjaro 'Kili' marathoni msimu huu wamekabidhiwa viwanja huko Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Wanaridha hao, Aloyce Felix Simbu na Anjelina John Tsere wamekabidhiwa viwanja hivyo katika hafla iliyoongozwa na rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT), Silas Isangi.

Wengine walioshiriki kwenye hafla hiyo ni nyota wa zamani wa riadha, Suleiman Nyambui na Juma Ikangaa sanjari na viongozi wa Chama cha riadha mkoa wa Dar es Salaam (DAA).

Akikabidhi hati za viwanja hivyo, Catherine Michael ambaye ni meneja masoko wa kampuni inayojihusisha na masuala ya viwanja nchini (SPC) amesema hiyo ni zawadi yao kwa wanariadha hao wanaokuja kwa kasi nchini.

"Tuliahidi kutoa zawadi ya viwanja kwa mabingwa wa Kili marathoni msimu huu, mchakato wa kupata hati umekamilika na leo  tumehimisha zoezi hili kwa kuwakabidhi viwanja hivyo ambavyo kila kimoja kina mita za mraba 400 na thamani ya Sh 4 Milioni kila kimoja," amesema.

Rais wa RT, Silas Isangi aliwashukuru SPC iliyoongozwa  na meneja mkuu, Neema Ally na Zena Matondo ambaye ni mkuu wa kitengo cha kukusanya madeni wa kampuni hiyo na kusisitiza kwamba riadha sasa ni ajira na si afya pekee kama ilivyozoeleka awali.

"Riadha kwa sasa sio afya tu, ni kazi inayowaingizia kipato wachezaji na kubadili maisha yao, kauli sawa na iliyotolewa na mkurugenzi wa mbio ya Kilimanjaro marathoni, John Bayo.

Bayo amesema zawadi hiyo ni hamasa kwa wanariadha nchini, na inatoa fursa kwenye mchezo huo na vijana kujiajiri.

Kwa nyakati tofauti, wanariadha hao wamesema hawakutarajia kupata zawadi hiyo huku wakisisitiza kuongeza juhudi zaidi ili kufika mbali.