Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kambi ya Simba noma, yazikwepa Al Ahly, Zamalek

JUMAPILI ya Agosti 8, Simba itakwea pipa kuelekea kambini kwenye mji wa Kifahari wa Alexandria nchini Misri. Alexandria inasifika nchini humo kama mji wa Kitalii na wenye maraha zaidi na ni miongoni mwa miji ghali Barani Afrika kwa muda mrefu.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ndani ya Simba tajiri Mohammed Dewji MO na Mtendaji, Barbara Gonzalez na Bodi ya Mnyama, wameamua kwenda kuweka kambi Alexandria ambako kuna utulivu na mazingira rafiki ya kujinoa zaidi ya Cairo.

Habari zinasema kwamba Simba imeamua kuweka kambi huko ili kukwepa msongamano wa Cairo ambako kuko bize saa 24 kutokana na umaarufu wa Uwanja wao wa ndege na vilevile ni Jiji kubwa la Kibiashara.

Cairo ndipo yalipo makao makuu ya Zamalek, Al Ahly na Ismailia ambako ni wakongwe wa soka la nchi hiyo na Afrika. Kutoka Cairo ambako Simba itatua ikitokea Dar es Salaam ni mwendo wa dakika 45 kwa ndege kufika Alexandria.

Kwa Gari Binafsi ni muda wa saa 2:30 kufika Alexandria. Mji huo umekuwa ghali kutokana na fukwe zake, utulivu, hali ya hewa na vivutio vingi. Simba itakaa kwenye mji huo ikinoa hadi Agosti 28 ambapo watacheza mechi kadhaa za kirafiki kujiweka sawa na Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza wikiendi ya kwanza ya Septemba. Ratiba ya michuano hiyo itakapangwa nchini Misri ila jijini Cairo na Simba bado itakuwa kambini hukohuko Arabuni. Simba imepania kufanya maajabu kwenye michuano ya kimataifa msimu huu ikiendelea zaidi ya robo fainali ilikoishia mara mbili mfululizo.

Tanzania msimu huu kwenye michuano hiyo itawakilishwa na Simba, Yanga huku Shirikisho wakienda Biashara na Azam.