Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kambi Simba kuhamishiwa uzunguni, mastaa kuoga manoti

NYOTA wa Simba wakimaliza dakika 90, kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya USGN kwa ushindi na kutinga robofainali kila mmoja akaunti yake itakuwa na mkwanja mrefu wa maana.

Mechi hiyo iliyopelekwa hadi Saa 4:00 usiku na mabosi wao kujipanga kwa usalama na hata usafiri kwa mashabiki huku wakisisitiza ni muda mzuri kwani utachezwa ndani ya Mfungo wa Ramadhani unaoanza kesho.

Kutokana na umuhimu wa mchezo huo mabosi wa Simba wamefanya mambo mawili, kuwatoa wachezaji kambi Mbweni na kuwapeleka Masaki ambako ni uzunguni zaidi, jambo la pili kuwatangazia bonasi ya maana itakayowapa motisha ya kushinda mechi.

Nyota wa Simba wakiwa wanasubiri ahadi ya bonasi, awali waliingia makubaliano ya kupokea pesa nusu ya bonasi zao kwenye Kombe Shirikisho Afrika na nusu waliambiwa watapokea mwisho wa hatua ya makundi wakiwa wametinga robo fainali.

Iko hivi. Mwanaspoti limepenyezewa, makubaliano yalikuwa wakishinda mechi ya nyumbani watapata bonasi Sh30 milioni ila watachukua nusu Sh15 milioni na nusu nyingine kuwekwa pembeni, wakishinda ugenini watapata Sh60 milioni na wakitoka sare watapata Sh30 milioni ila watachukua nusu.

Kwa matokeo ya Simba yalivyo kwenye Kundi D kabla ya mchezo wa mwisho, imeshinda mbili nyumbani, hivyo ikawekwa Sh30 milioni kando, walitoka sare ugenini ikawekwa Sh15 milioni pembeni.

Ni kazi kwao mastaa wa Simba kutinga robo fainali itakayowafanikisha kupata Sh45 milioni, kama walivyokubaliana na viongozi wao, pesa hiyo bonasi watapewa kwa kufuzu makundi.

Mbali na mkwanja huo (Sh 45 milioni), mechi ya Jumapili dhidi ya USGN inajitegemea bonasi kwa umuhimu wake hazitaingilia na zile nyingine za makundi.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti zinasma mabosi wametenga si chini ya Sh60 milioni ili kuongeza motisha ya kila mchezaji.

Hivyo kama Simba itashinda maana yake wachezaji watakuwa na uhakika wa kuvuta Sh105 milioni ila kwenye mgao itakuwa tofauti kwa kila mchezaji.