Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kabwili ajitoa Yanga kimtindo

Muktasari:

Kipa huyo aliiongoza Serengeti Boys katika mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana yaliyofanyika Gabon

Dar es Salaam. Kipa chipukizi wa Yanga, Ramadhan Kabwili amesema ili kiwango chake kirejea atakuwa anadaka mechi zote zinakazochezwa na kikosi B.

Kabwili alisema ameuomba uongozi wa timu hiyo kila inapotokea michezo ya kirafiki katika timu yao ya vijana waweze kumpa nafasi ya kwenda kudaka ili kuimarisha ubora wake.

Alisema ushindani wa namba katika kikosi cha kwanza kinachoongozwa na kipa Mkongo Klaus Kindoki na Beno Kakolanya ni mgumu kwake japo ananafasi ya kucheza na ndio maana ameona aombe kucheza michezo ya kikosi B ili kuendelea kujiimarisha zaidi.

"Sijashushwa kikosi B ila mimi ndiye niliyeomba micheze mechi za kirafiki za timu ya vijana ili kujiimarisha zaidi ili niweze kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mwinyi Zahera jambo ninaloamini linawezekana."

Kabwili aliongeza kuwa anaamini kupitia michezo atakayopata kucheza itamsaidia kuongeza uimara na ujasiri wa kukaa langoni kwa kujiamini na kuendelea kujiimarisha zaidi.