Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Azam, Manula yafikia hapa

Muktasari:

  • Taarifa za uhakika ilizopenyezewa Mwanaspoti ni kwamba, Manula alipasa kusaini mkataba Alhamisi baada ya  kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Aga Khan akiwa sambamba na kiungo Muhsin Malima ambaye naye inaelezwa anajiandaa kusaini mkataba wa kuitumimkia timu hiyo.

PILIKAPILIKA za usajili wa wachezaji wapya katika vikosi vya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine ya soka nchini na nje ya nchi zimeanza kushika kasi, lakini wakubwa wa Bara wanapambana kwelikweli kuhakikisha kwamba wananasa saini za mastaa wapya, ingawa kila kitu kinakwenda kimyakimya.

Dirisha la usajili wa wachezaji ambalo linatarajiwa kufunguliwa mara tu mashindano ya soka nchini yatakapomalizika mwezi huu, huenda Ligi Kuu Bara msimu ujao ikaja na sura mpya za mastaa katika timu mpya.

Tayari mabosi wa Azam FC wameanza mipango ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao ikielezwa ipo hatua ya mwisho kumsainisha mkataba, kipa wa Aishi Manula, sambamba na kumbeba kiungo mahiri aliyekuwa akicheza soka la kulipwa huko Misri.

Taarifa za uhakika ilizopenyezewa Mwanaspoti ni kwamba, Manula alipaswa kusaini mkataba Alhamisi baada ya kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Aga Khan akiwa sambamba na kiungo Muhsin Malima ambaye naye inaelezwa anajiandaa kusaini mkataba wa kuitumimkia timu hiyo.

Azam imemrejesha Manula baada ya kipa huyo kuihama 2027 kujiunga na Wekundu hao ambao hata hivyo kuanzia msimu uliopita benchi la ufundi limeonyesha kutompa nafasi kikosini, hususani msimu huu ambapo hajacheza mechi hata moja ndipo menejimenti yake imeamua kumrejesha Chamazi.

Manula amekosa nafasi ya  kucheza kwenye kikosi cha Simba msimu huu huku nafasi yake akicheza Moussa Camara ambaye ameonyesha kiwango kizuri na hadi sasa ndiye kinara wa kutoruhusu mabao (clean sheet) 17 katika mechi 25 alizocheza hadi sasa katika Ligi Kuu.

Mwanaspoti lilimshuhudia Manula akiwa sambamba na kiungo mshambuliaji, Muhsin Malima katika Hospitali ya Agakhan iliyopo Posta wakiwa sambamba na baadhi ya watu kutoka Azam waliokuwa wanasimamia zoezi hilo.

Muhsin yeye alikuwa anacheza soka la kulipwa Misri katika klabu ya Zed FC lnaye amesaini katika klabu ya Azam.

Habari kutoka kwa watu wa karibu na uongozi wa Azam, zimelidokeza Mwanaspoti kumalizana na wachezaji hao na wataitumikia timu hiyo msimu ujao.

“Walikuwapo pale Aga Khan wakipimwa afya, nadhani tusubiri tu watambulishwe muda wowote maana wote ni wachezaji huru,” kilisema chanzo hicho.

Aidha, chanzo cha karibu cha wachezaji hao kilisema; “Wachezaji hao kesho (leo) Alhamisi) watasaini mikataba yao ya kuitumikia timu hiyo. Upande wa Muhsin yeye alikuwa anakaa Mbande, lakini amehama na sasa yupo karibu na Uwanja wa Azam Complex ambao wanautumia Azam.”

Manula anarejea Azam baada ya ukosekana katika kikosi hicho kwa miaka tisa tangu alipoondoka 2017 na kuiwezesha Simba kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho mbili na Ngao ya Jamii tano na Kombe la Mapinduzi moja.

Pia akiwa Simba alikuwa sehemu ya kikosi kilichofika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara nne na kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, japo hakutumika hata mechi moja wakipoteza mbele ya RS Berkane na anarudi Azam aliowahi kubeba nao ubingwa wa Ligi 2013-2014.

Mwanaspoti liliwasiliana na Mkuu wa Idara ya Habari ya Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ili kupata ufafanuzi huu ya taarifa hizo za usajili wa nyota hao wawili, lakini alisema hakuwa na taarifa yoyote kwani aanachojua ishu za usajili zitaanza kufanywa baada ya kumalizika kwa msimu.