Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

India Kabbadi bingwa Jumuiya ya Madola

KABBADI Pict

Muktasari:

  • Matokeo ya timu ya India wanawake yalikuwa kama ifuatavyo; India 35-15 Uganda, India 73-13 Malaysia, India 32-16 Singapore, India 41-18 Uganda, 38-10 Nigeria, India 39- 14 Sri Lanka.

TIMU za India kwa mchezo wa Kabaddi wanaume na wanawake, zimetwaa ubingwa katika mashindano Jumuiya ya Madola yaliyofanyika nchini humo.

Timu ya wanaume imetwaa ubingwa huo kwa kuifunga Sri Lanka pointi 54-20, mchezo wa fainali ya mashindano hayo huku wanawake ikiifunga Uganda pointi 35-15.

Licha ya kutwaa ubingwa huo, timu ya India kwa wanaume imekuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote kuanzia hatua ya makundi hadi kufika fainali.

Matokeo ya India wanaume yalikuwa hivi; India 54-20 Sri Lanka, India 46-26 England, India 44-30 Uganda, India 37-23 Malaysia, India 50-23 Nigeria, India 48-20 Tanzania, India 45-24 Sri Lanka, India 56-27 Bangladesh.

Timu ya Kenya wanaume na wanawake zote zimeishia kwenye hatua ya nusu fainali ya maishndano hayo baada ya kufanya vizuri katika makundi.

Tanzania imemaliza kwenye nafasi ya tano ya kundi A, ikicheza mechi sita ikifanikiwa kushinda mbili na kupoteza nne, wakati Nigeria ikimaliza ya mwisho kwa kundi hilo bila kupata ushindi wowote sawa na Australia ikiwa kundi B.

Pia timu ya wanawake ya India imeandika rekodi yake ya kutofungwa katika mchezo wowote tangu kuanza kwa mashindano hayo hadi kufikia hatua ya fainali.

Matokeo ya timu ya India wanawake yalikuwa kama ifuatavyo; India 35-15 Uganda, India 73-13 Malaysia, India 32-16 Singapore, India 41-18 Uganda, 38-10 Nigeria, India 39- 14 Sri Lanka.