Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hope City Deaf bingwa ligi ya viziwi Zanzibar

HOPE Pict

Muktasari:

  • Ligi hiyo ya viziwi Zanzibar msimu huu 2026-2027 ukiwa wa kwanza ilishirikisha timu nne ambazo ni bingwa Hope City Deaf, Wakombozi, Vuka Deaf na Zandeaf zote za Unguja.

TIMU ya Hope City Deaf imefunga msimu kwa kishindo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Viziwi Zanzibar katika fainali iliyochezwa Oktoba 3, 2026 kwenye Uwanja wa Mao, Unguja.

Hope City Deaf imetwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Wakombozi bao 1-0, lililofungwa na Bakari Rashid dakika ya 28.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar, Abuubak Said Lunda, aliipongeza Hope City Deaf kwa kutwaa ubingwa huo.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na timu hiyo kwa lengo la kuimarisha ligi hiyo msimu ujao, ikiwemo kuongeza idadi ya timu na kusimamia vipaji vya wachezaji viziwi.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Namala Suleiman, amesema wamefurahi kumaliza ligi salama huku wakishuhudia hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki.

Alitoa wito kwa wadau na wafadhili kuiunga mkono timu ya Taifa ya Zanzibar ya viziwi, inayotarajiwa kwenda Ethiopia kushiriki mashindano ya kimataifa.

Ligi hiyo ya viziwi Zanzibar msimu huu 2026-2027 ukiwa wa kwanza ilishirikisha timu nne ambazo ni bingwa Hope City Deaf, Wakombozi, Vuka Deaf na Zandeaf zote za Unguja.