Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hasnath Ubamba afanya maajabu Misri, mkataba mpya wanukia

ASNAT Pict

Muktasari:

  • Ubamba alijiunga na FC Masar Julai 30, 2024 kwa mkataba wa miaka mitatu na tangu hapo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho kinachotamba kwenye Ligi ya Wanawake Misri.

KUTOKANA na kiwango kikubwa anachoendelea kukionesha winga mbongo, Hasnath Ubamba katika kikosi cha FC Masar, uongozi wa klabu hiyo umeanza mchakato wa kumboreshea mkataba wake kabla ya kumalizika mwaka 2027.

Ubamba alijiunga na FC Masar Julai 30, 2024 kwa mkataba wa miaka mitatu na tangu hapo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho kinachotamba kwenye Ligi ya Wanawake Misri.

Tangu amejiunga na timu hiyo, amecheza misimu miwili ya ushindani mkubwa na amekuwa mchezaji muhimu kwenye eneo la ushambuliaji akiisaidia timu hiyo  katika mashindano ya ndani na michuano ya Afrika.

ASN 01

Katika msimu wake wa kwanza (2024/25), Ubamba alifunga mabao sita ya ligi na mawili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake . Uchezaji wake wa utulivu na uwezo wa kucheza nafasi za ushambuliaji ulimfanya kuwa miongoni mwa wachezaji waliopata nafasi ya kudumu kikosini.

Kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa aliisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu akiwa miongoni mwa nyota waliobeba tuzo ya mchezaji bora wa mechi mara moja.

ASN 02

Mwaka huu pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu kuishia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa akifunga mabao matatu na asisti moja.

Juzi timu hiyo imeandika historia mpya baada ya kutwaa tena kombe la ligi baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wapinzani wao Wadi Degla katika fainali iliyopigwa Misri, taji hilo linakuwa la tatu mfululizo kwa Ubamba na kumfanya awe miongoni mwa nyota wa Kitanzania aliyecheza michuano ya Afrika mara nyingi zaidi .

ASN 03

Ushindi huo unakamilisha msimu wa mafanikio makubwa kwa FC Masar, ambao sasa wanathibitisha ubabe wao ndani ya soka la wanawake Misri baada ya kutwaa mataji mawili makubwa msimu mmoja ligi na kombe la ndani.