Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guede atupia tena, Singida ikiibana Azam

GUEDE Pict

Muktasari:

  • Guede amefunga bao hilo dakika ya 75 akiitumia vizuri pasi ya kisigino kutoka kwa Idriss Diomande, katike mechi ya Kundi A kunako Kombe la Mapinduzi 2026 iliyochezwa Desemba 31, 2025 kuanzia saa 2:15 usiku.

MSHAMBULIAJI Muivory Coast, Joseph Guede ameibuka mkombozi wa kikosi hicho baada ya kuisawazishia bao katika sare ya 1-1 dhidi ya Azam.

Guede amefunga bao hilo dakika ya 75 akiitumia vizuri pasi ya kisigino kutoka kwa Idriss Diomande, katike mechi ya Kundi A kunako Kombe la Mapinduzi 2026 iliyochezwa Desemba 31, 2025 kuanzia saa 2:15 usiku.

Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 69, mfungaji akiwa Jephte Kitambala.

Kitambala alitumia vizuri makosa ya walinzi wa Singida Black Stars sambamba na kipa, Metacha Mnata ambao kwa pamoja walikwenda kuiwahi pasi mpenyezo ya Sadio Kanoute, lakini wakajikuta wanagongana na mpira kumkuta mfungaji aliyemalizia kirahisi.

Kabla ya kuingia kwa mabao hayo, mechi ilitawaliwa na kosakosa za hapa na pale huku makipa wa pande zote, Metacha na Aishi Manula wa Azam wakikaa imara langoni.

Imeshuhudiwa katika mechi hii, Singida Black Stars ikimtumia Ibrahim Imoro ambaye imemrudisha kundini baada ya kumtoa kwa mkopo dirisha kubwa la usajili kwenda Mtibwa Sugar.

Kocha wa Azam, Florent Ibenge naye alitumia baadhi ya sura mpya ndani ya kikosi hicho akiwamo Ilese Kolonga Caleb na David Bela Bakwayima wote raia wa DR Congo.

Sare hiyo imeifanya Azam kuwa na pointi moja ikicheza mechi moja, huku Singida ikiendelea kuwa kileleni na pointi nne. Imebakiwa na mechi moja dhidi ya URA itakayochezwa Januari 3, 2026.

Azam mechi mbili hatua ya makundi zilizobaki ni dhidi ya Mlandege (Januari 2, 2026) na URA (Januari 5, 2026).

Kwa upande mwingine, Guede amefikisha mabao mawili, ndiye kinara kwa sasa baada ya mechi ya kwanza kufunga katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mlendege.