Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita sasa yamtaka Chasambi

Muktasari:

  • Geita Gold inataka Chasambi kwa lengo la kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

GEITA Gold imeanza kupiga hesabu za kuboresha zaidi kikosi hicho, huku ikimtaka winga wa zamani wa Simba ambaye hivi karibuni amechukua uamuzi wa kuvunja mkataba na Singida Black Stars, Ladack Chasambi.

Geita Gold inataka Chasambi kwa lengo la kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Mmoja wa viongozi wa Geita aliliambia Mwanaspoti kuwa, wanamtaka winga huyo ikiwa ni mapendekezo ya kocha Zuber Katwila, anayetaka kutafutiwa winga mwenye kasi.

Chasambi hakuwa na wakati mzuri na Singida ambayo ilimsajili msimu huu akitokea Simba, ambako pia hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, Geita inaamini bado Chasambi ni mchezaji bora ambaye kama atakutana na kocha wa timu hiyo, atamrudisha kwenye kiwango chake bora kama ambavyo alikuwa awali kwenye timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

“Tunatafuta winga kweli na yule Chasambi ni chaguo letu namba mbili, kuna winga tunamtaka kwa mkopo kama tukimkosa basi tutaondoka na Chasambi yule bado ni mchezaji mzuri licha ya changamoto anazokabiliana nazo,”alisema kiongozi huyo wa Geita.

“Bado umri wake ni mzuri lakini unajua tuna kocha ambaye amepita Mtibwa na anamjua Chasambi, tunaamini atakuwa amerudi kwa kocha sahihi ambaye atarudisha uwezo wake.”

Geita Gold imekuwa katika mwenendo usioridhisha, ikiwa imecheza mechi 11, imeshinda mbili, sare tatu na kupoteza sita, huku ikikusanya pointi tisa zinazoiweka nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi.

Katika mechi 11 ilizocheza, Geita Gold imefunga mabao 11 na kuruhusu 18, ikiwa na tofauti ya mabao saba hasi. Kwa wastani, timu hiyo inafunga bao moja kwa mchezo huku ikiruhusu mabao 1.6.