Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Feisaly aponda kumvimbisha kichwa nyota Simba

Muktasari:

  • Fei amesema hapendi kuzungumza sana ila kwake ni vitendo na kubainisha kuwa siku zilizobaki kuelekea msimu mpya wa ligi ni chache hivyo mashabiki wanapaswa kusubiri ndani ya dakika 90.

WAKATI kiwango cha kiungo wa Simba, Claytous Chama kikionekana kuwa tishio kwa wapinzani wao lakini nyota wa Yanga, Feisaly Salum 'Fei toto' ameshangazwa na sifa hizo na kutamka kuwa mashabiki ndio wataamua nani bora kati yake na staa huyo wa Msimbazi kutoka Zambia.

Fei amesema hapendi kuzungumza sana ila kwake ni vitendo na kubainisha kuwa siku zilizobaki kuelekea msimu mpya wa ligi ni chache hivyo mashabiki wanapaswa kusubiri ndani ya dakika 90.

Alisema yupo fiti kwa mapambano na viungo wa timu pinzani huku akiweka wazi kuwa kubwa analotaka kulifanya ni kuhakikisha timu yake inapata matokeo mazuri katika kila timu watakayokutana nayo.

"Sipendi kuzungumzia timu moja wakati ligi ina timu 20 natambua Simba ndio wapinzani wetu na ndio timu ambayo imekuwa ikiangaliwa kwa ukaribu zaidi kutokana na kushikilia ubingwa. Hivyo napambana kuhakikisha nairudisha timu yangu kwenye makali ya misimu mitatu iliyopita kwa kusaidiana na wenzangu," alisema Fei.

Fei Toto alisema mchezaji yeyote anayejua anachokifanya hawezi kuogopa upinzani hivyo kutokana na uwezo alionao anataka aonyeshe kile anachoamini ndio kitaisaidia timu yake kufanya vizuri kwenye ligi.