Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto: AS Vita ni kipimo sahihi kwa nyota wapya Yanga

Muktasari:

Fei Toto amejiunga kambini leo akitokea mapumzikoni baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya Taifa Taifa Stars.

Dar es Salaam. Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema mchezo wao dhidi ya AS Vita ni kipimo tosha kwao kuonyesha ubora wa nyota wapya waliosajiliwa na kudhihilisha maandalizi waliyofanya.

Fei Toto ameungana na kikosi Morogoro leo baada ya mapumziko ya wiki mbili waliyopewa kutokana na kutoka katika majukumu ya timu ya Taifa Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki mashindano ya AFCON, Stars haikufanikiwa kushinda mechi hata moja.

Fei Toto alisema aliposikia taarifa za kukutana na AS Vita alifurahia kwani aliamini ni mchezo ambao utaonyesha mwanga wa ubora wa kikosi chao kabla ya Ligi Kuu aijaanza huku akibainisha kuwa ndio mchezo utakaotoa taswila nani yuko fiti.

"Ni timu kubwa na bora itasaidia kwa namna moja au nyingine kutuonyesha nani ni bora zaidi ya mwenzake naamini mwalimu atatoa nafasi kwa nyota wote kucheza katika mchezo huo kwa lengo la kusuka kikosi chake bora cha ligi msimu unaokuja."

"Bado sifanya mazoezi na nyota wapya waliosajiliwa Yanga kujua ubora wao japo kuna ninao wafahamu kama Makame ambaye nimeshacheza naye naamini muda ukifika kila mmoja atajionea ubora wa mmoja mmoja," alisema Fei Toto.