Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu atuma agizo zito kwa mabosi wa Yanga

FADLU Pict


KOCHA Mkuu wa Yanga, Fadlu Davids, ameanza kuweka wazi mipango yake ya muda mrefu ndani ya kikosi hicho kwa kuwataka mabosi wa klabu hiyo kuhakikisha wanambakiza beki wa kushoto, Chadrack Boka, kwa kumuongezea mkataba mpya.


Boka alijiunga na Yanga Julai 7, 2024, akitokea FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, akipewa jukumu la kurithi nafasi ya Mkongomani mwenzake, Joyce Lomalisa aliyekuwa akiondoka Jangwani. Beki huyo alipewa mkataba wa miaka miwili na nusu ambao unatarajiwa kufikia ukingoni Januari 2027.


Katika kipindi chake Yanga, Boka amejijengea nafasi kutokana na kasi yake, uwezo wa kupandisha mashambulizi na kujituma katika majukumu ya ulinzi. Alianza kuonyesha thamani yake mapema na kuwa miongoni mwa mabeki waliotegemewa na makocha waliopita, licha ya ushindani aliokuwa akiupata katika nafasi yake

FAD 01

Mwanaspoti linafahamu kuwa, Fadlu amewaeleza viongozi wa Yanga kuwa Boka ni miongoni mwa wachezaji anaowahitaji katika mfumo wake wa kiuchezaji, akiamini uwezo wa beki huyo wa kupandisha mashambulizi kupitia pembeni, kutengeneza nafasi na kufanya majukumu ya ulinzi unampa thamani kubwa kikosini.

Fadlu alikuwa na nia ya kufanya kazi na Boka tangu alipokuwa Raja Casablanca ya Morocco, ambapo aliwahi kuonyesha kuvutiwa na huduma ya beki huyo. Sasa akiwa Yanga, amewaeleza mabosi wake kuwa anahitaji kuendelea kuwa naye badala ya kumruhusu aondoke.

Taarifa za ndani zililieleza Mwanaspoti kuwa: “Kutokana na msimamo huo, Yanga tayari imemuita nchini meneja wa Boka ili kuanza na kukamilisha mazungumzo ya kuongeza mkataba wa beki huyo.

“Sababu kubwa inayomfanya Fadlu kutaka Boka abaki ni aina ya uchezaji wa beki huyo, ambaye si mlinzi anayesubiri kushambuliwa pekee, bali ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi kupitia upande wake.”

FAD 02

Mapema msimu huu, kulikuwa na taarifa kuwa, Azam ilikuwa kwenye hesabu za kumsajili beki huyo ili akaongeze nguvu kwenye eneo la kushoto ambapo kocha wa kikosi hicho, Florent Ibenge ndiye aliyependekeza usajili huo kwa viongozi, hata hivyo dili hilo halikufanyika.

Tangu alipojiunga na Yanga, Boka amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya kikosi hicho kwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo katika misimu ya 2024-2025 na 2025-2026, Kombe la Shirikisho (FA) la msimu wa 2024-2025, na Ngao ya Jamii misimu mitatu mfululizo huku akichangia bao muhimu mwaka 2024.

Katika nafasi ya beki wa kushoto Yanga, Boka anakutana na ushindani wa moja kwa moja kutoka kwa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, aliyesajiliwa Agosti 2025 kutoka Simba.

Tshabalala ni beki mwenye uzoefu wa ligi ya Tanzania na mashindano ya kimataifa, jambo linalomfanya Boka asipate nafasi ya kupumzika katika vita ya kupambania namba.